Vitu vitano (5) vitakavyokusaidia kufanikiwa katika eneo lako la biashara.

Leo nataka nikupe siri 5 za vitu ambavyo ni vya kawaida sana tunavyovifanya kila siku katika maisha ya kawaida lakini tunavifanya aidha kwa mazoea au kwa kurithi leo nnakupa mwanga na sababu kadhaa za kwanini unatakiwa kuziwekea mkazo hizo sehemu au vitu hivyo kwa manufaa ya biashara yako, katika Branding hakuna kitu kipya ambacho utakutana nacho ila utakutana na elimu ya jinsi ya kutumia vitu kwa usahihi ili vilete malengo chanya katika biashara yako.Jifunze branding mara nyingi uwezavyo ni msingi au mhimili wa bishara yako.


1. Waza tofauti (Ushindani ndio biashara)

Katika vitu vitano (5) ambavyo ukivishika vizuri na kuvifanyia kazi kwa umakini vitakusaidia kufanikiwa katka eneo la biashara yako ni jinsi unavyowaza, mawazo yako ni hazina kubwa katika biashara yako. Unatakiwa kama mfanyabiashara au mjasirimali  uwe na mawazo chanya uone nafasi kwenye changamoto(tatizo) kwenye kila hatua kitu kikubwa kinacho waangusha wengi ni kuchukulia changamoto kama tatizo hivyo hujikuta hata changamoto ndogo inakurudisha nyuma sehemu kubwa,mhimili mkubwa wa biashara yako  upo katika mawazo kuna wafanyabiashara wengi/wajasiriamali hata ushindani katika biashara kwao ni tatizo, lakini kama mfanyabiashara/mjasiriamali unatakiwa utambue biashara ni ushindani na ushindani ni changamoto hivyo siku zote usichukulie ushindani katika hali ya tatizo ila hali ya changamoto ambalo ni daraja unajijengea mwenyewe kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine. Waza tofauti na washindani wenzako ili uzione fursa.


2. Zidisha umakini kwenye mahusiano yako.

Ukiwa kama mfanyabiashara au mjasiriamali mahusiano yako na vitu au watu tofauti tofauti nje na ndani ya biashara yako ni jambo la msingi na muhimu sana, mahusiano yanajumlisha,mawasiliano huduma,ufanisi,mapenzi nakadhalika, lakini sehemu ambazo unatakiwa uzidishe mahusiano na wewe mwenyewe ni pamoja na,


I. wewe na  biashara yako

Ni lazima wewe mwenyewe kwanza uwe na mahusino mazuri na biashara yako unayoifanya kwa sababu wewe ndio umebeba sura na muonekano wa biashara yako, kama hautakuwa na mahusiano mazuri na biashara yako basi ni lazima italeta shida ninaposema mahusiano na bashara yako namaanisha wewe kuijua vizuri biashara yako na kuendana nayo (Chemistry) unapotengeneza mahusiano mazuri na biashara yako ni nafasi nzuri unayompa mteja wako kukuamini na pia kuipenda biashara yako.


II. wewe na mteja wako.

Mteja ndio anapewa nafasi ya kwanza katika biashara lakini huku anakuwa nafasi ya pili sababu bila kuwa na mahusiano mazuri na biashara hauwezi ukapata wateja, mahusino mazuri na mteja ni pamoja na unavyomhudumia, unavyoongea nae unavyowasiliana nae nakadhalika, mteja wako ni mtu wako wa masoko hivyo ukiwa na mahusiano mazuri na mteja wako unakuwa unaongeza nafasi ya mteja kukufanyia marketing kwa wenzake anaokutana nao.


III. Mahusiano yako wewe na washindani.

Biashara sio vita ni mchezo  wa kutumia akili nyingi, baada ya kutengeneza mahusiano mazuri na biashara pamoja na mteja ni vizuri sana kuwa na mahusiano mazuri na washindani wako pia kama ambavyotulisha angalia aina za washindani vivyo hivyo ukiwa na mahusiano mazuri nao utapata nafasi za kutambua vizuri na pia kujua mbinu na mipango ambapo wewe itakusaidia kujitengeneza na kujiunda tofauti na   wao.
Hivyo kusimamia mahusiano hayo matatu inafaida kubwa sana katika biashara yako.


3.Jifunze kufanya kazi kwa umakini zaidi ya kufanya kazi kwa nguvu.

 Biashara inahitaji akili nyingi kuliko nguvu hivyo weka umakini wako mwingi katika biashara, sio nguvu zako nyingi katika biashara japo nguvu inahitajika ili kuleta ufanisi wa kazi, katika biashara vitu huwa vinaumbwa kwanza kichwani kisha vinadhihirishwa katika ulimwengu wa biashara lakini iwapo hautakiumba kichwani kitafanyikaje na kwa namna gani ukategemea kitakavyokuwa ndio matokeo yake unatumia nguvu nyingi bila kujua matokeo yake, hivyo nguvu inahitajika lakini nguvu isiwe nyingi kuzidi akili.Ukifungua akili katika mengi utafunguka vingi kama ile siri ya kwanza waza tofauti ukiweza kuwaza tofauti basi unauwezo mkubwa wa kufanya vingi, usitumie nguvu nyingi sehemu ya kutumia akili itakugharimu ilhali utakuwa umeshagharimika.


4. Wasiliana , Sikiliza na Changia

Moja kati ya matatizo makubwa yanayoisumbua nchi yetu na dunia nzima ni mapokeo ya mawasiliano, watu wengi husikiliza na kupokea mawasiliano ili atoe jibu japo maana na dhana kuu ya kuwasiliana ni kuelewa,lakini imeshakuwa kasumba tunasikiliza ili tujibu, mawasiliano ni kitu muhimu sana hii fomula nilioandika kama kichwa cha kipengele hiki itakusaidia kuimarisha eneo hilo, jifunze kuwasiliana na dhana kuu ya mawasiliano ni kuelewana sio kujibizana, na katika biashara unatakiwa umuelewe mteja ndio umjibu,kuna aina nyingi za mawasiliano sio kuongea peke yake kuna ishara,vitendo, hisia, kuongea nakadhalika., Pia jifunze kusikiliza na kuelewa, usisikilize ili ujibu sikiliza na kuelewa kisha changia , usijibu changia kwanza ili kushibisha ulichokielewa na kuipata maana lengwa na unayewasiliana nae ndio ujibu iwapo itahitaji jibu lako.


5.Ongeza juhudi katika mafanikio

Mwisho kabisa kwa leo ni kuongeza bidii na juhudi katika mafanikio, mafanikio yapo ya aina mbili kuna mafanikio yanayoonekana na yasiyoonekana mafanikio yanayoonekana ni matokeo ya mafanikio yasiyoonekana,hivyo usipuuze mafanikio yasiyoonekana na au kuona mafanikio flani ni madogo au hayaonekani ongeza juhudi  na juhudi zako zitainua mafanikio yasiyoonekana kuleta mafanikio yanayoonekana. Mfano: hata unapotuma maombi ya kuomba kazi ukifanikiwa kuitwa katika usahili yale ni mafanikio lakini ukifeli katika usahili haimaanishi hauna mafanikio, unatakiwa uyachukulie yale mafanikio ya mwanzo yakupe moyo kwamba hata kama sijafanikiwa lakini ninavigezo vya kuitwa kwenye usahili.

Iwapo utapenda kuwa unapokea matoleo yangu kwa njia ya barua pepe nitumie anwani yake yako ya barua pepe kwenda namba tajwa hapo chini na pia wale watakaopendelea kuunganishwa katika kundi la Whatsapp Branding,tuma namba yako ya simu na jina kwenda namba 0684047323. Pia unaweza kunifuatilia kupitia ukurasa wa facebook (Elisha Chuma) Asante.







Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango