Vitu vya kuzingatia unapotaka kuanza au ukiwa mjasiriamali ili ufanikiwe.
Kwanza niwape hongera ambao tayari wameshafanikiwa kupata
vitambulisho vya kupigia kura kwa nchi nzima na niwape pole kwa wale ambao bado
hawajapata na pia nnawatia moyo kuendelea kuvifuatilia vina maana sana kwa
maisha yako naya kizazi chako cha sasa na cha baadae.
Baada ya kutoa salamu hizo sasa nirudi kwenye mada kuu leo
hapo juu, taifa letu linapoteza sana nguvu kazi ya taifa katika vitu ambavyo
havina mafanikio na malengo chanya kwa maisha ya mhusika na taifa na kutokana
na kupunguza umakini katika hilo sasa hivi tumejikuta vijana wengi wanamaliza
mafunzo ya elimu zao lakini hawana kazi wanabaki kuwa omba omba na wadandiaji
wa kazi wasizokuwa na weledi nazo.
Leo nitaongelea kwa upande wa wajasiriamali wadogo ambao
wanafanya biashara ndogo ndogo kwa minajili ya kupata kipato cha kuendesha
maisha yao ya kila siku na wale ambao wanafikira kuingia katika ujasiriamali au
biashara. Asilimia kubwa sana ya vijana wanafeli katika biashara na
ujasiriamali kwa kukosea baadhi ya vitu ambavyo walitakiwa wavifahamu mapema
lakini wanajikuta vinawarudisha na nyuma na kufeli. Katika hali ya kawaida
unaweza kuona kama hakuna kilichopotea lakini ukiangalia kwa undani utaona
umepoteza muda,ufanisi,mali na hata malengo kwa ajili ya kutegemea kitu ambacho
haukuwa na malengo nacho.
Baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na :-
1. MUDA

2. MALENGO
Baada ya kuangalia muda sasa tunakuja pacha wake malengo.Malengo
katika biashara au ujasiriamali ni muhimu sana lakini kwa wajisiriamali wadogo
wadogo wengi wao huwa hawana malengo ila wana matarajio hawaweki malengo kwa
ajili ya ujasiriamali au biashara yao wao wanasubiri matarajio ya biashara
yenyewe itakavyokuwa unapofanya biashara au ujasiriamali ni sawa na unaingia
vitani hauwezi kuingia vitani unategemea vita itaamua mimi napambana tu, halafu
uje ushinde kwa kishindo japo kuna wenye bahati vita ikawa ni nyepesi ukashinda
lakini kwa vile ushindi wako ni mwepesi huwezi kupata fundisho kutokana na vita
hiyo ni rahisi sana kwa wewe kubweteka na ushindi kwa kujiona unaweza kumbe
umekutana na mvua nyepesi siku adui akirudi kwa ajili ya vita utashindwa vibaya
.nimeelezea dhana nzima ya kwann uweke malengo katika ujasiriamali au biashara
yako mapema sababu biashara ni vita.
3. UJASIRI
Ujasiri kama neno ujasiriamali lilivyo unatakiwa ujasiri wa
hali ya juu kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara hasa unapoanzisha biashara yako
ni ngumu sana kufanikiwa mara moja tu unapoanza hivyo ujasiri unatakiwa sana
katika kupambana na changamoto za biashara au ujasiriamali na kitu kibaya
ambacho huwa kinatokea ni kwamba biashara zinazotengenezwa huwa zinakuwa ziko
nje ya weledi wa mhusika mfano dokta atafungua duka la mahitaji ya nyumbani, au
aliesomea ualimu anaenda kuwa dreva anakuwa anafaya kama kwa kujishikiza au kwa
muda mfupi hivyo ujasiri wako unakuwa unapungua kutokana na akili unavyokuwa
umeiaminisha,Ujasiri wako ndio unaokuweka juu kwenye soko uwzo wa kupambanua na
kutatua vizuizi ndio unaokusimamisha sokoni hivyo kama mjasiriamali
anapungukiwa na ujasiri mwisho wake ni kufeli.
4. MFUMO
Hapa katika mfumo ni
sehemu kubwa sana, ambapo mfumo wetu wa kibiashara ndani ya nchi haumpi
nafasi sana mjasiriamali mdogo, mfumo wetu wa kibiashara unampa unafuu zaidi
mwenye uwezo kubwa hivyo kwa wajasiriamali wadogo ikitokea akaingia sokoni
anajikuta mfumo umemtupa mkono lakini hadi agundue kama mfumo umemtupa mkono
tayari anakuwa ameshawekeza nguvu na fedha ndani yake, tayari hilo linakuwa ni
tatizo.
5. MAISHA YA KUIGA

6. ELIMU
Asilimia kubwa ya wajasiriamali hawana elimu ya ujasiriamali
wanakuwa na elimu ya kufikiria hili ni tatizo ndio maana sasa hivi wengine
wameona ni mtaji ukiwa na elimu ya kufikiri utaitumia kufikiri kipi ni sawa na
kipi sio sawa lakini ukiwa na elimu ya ujasiriamali unakuwa na elimu ya
kutambua nifanye nini kwa muda gani na matokeo yake ni nini? Na pia hata
kuziona fursa zinapotokea kuliona tatizo kama changamoto kulitatua
kijasiriamali “ Mfano, nilisoma katika kitabu Fulani kulikuwa na biashara 3
zinazotoa huduma inayofanana, baada ya biashara kuwa mbaya kwa kipindi kirefu
mwenye biashara ya kushoto aliandika punguzo 20% akaanza kupata wateja kwake
baada ya muda na yule wa kulia akashusha punguzo 30% wateja wakawa wanaenda na
kwake hebu jifikirie ukiwa kama mfanyabiashara wa katikati utafanya
nini?.......ambapo alieweka 30% anauza kwa bei ya kurudisha gharama hakuna faida,
(Ntasubiri jibu lako kwenye sehemu ya komenti chini ).hivyo unapokosa elimu
sahihi kwa kitu sahihi ujue mafanikio yake ni ya kubahatisha sio ya lazima.
Hitimisho.
Kwa leo naishia hapo ushauri wangu kwa wajasiriamali kwanza
wanatakiwa wapate elimu ya ujasiriamali ili waweze kuuelewa mfumo wa kibiashara
ambao utawapa ujasiri wa kupanga na kusimamia malengo kulingana na muda
Jibu la mfano hapo juu litatoka ndani ya komenti zitakazowekwa hapa chini.Yule mfanyabiashara wa katikati alifanya nini?
Kujiunga na kundi la whatsapp branding tuma namba na jina lako kwenda namba 0684047323 (Whatsapp sms tu), pia unaweza kunipata kwa ukaribu zaidi kwa kuniandikia email(elishachuma@gmail.com) au like page yangu Elisha Chuma.
Comments
Post a Comment