Je! unajua maana ya Meme/Motto/Slogan katika biashara yako?

Watu wengi wamekuwa wanafanya vitu bila kutambua maana na kwanini, leo nitatoa dondoo kidogo kuhusu meme/Slogan/Motto. Hiki sio kitu kigeni lakini wengi tumwekuwa tukikifanyia mazoea leo pata darasa kidogo. Kila biashara inapofanyiwa branding lengo kuu liko kwa mteja na unapotaka kumpata mteja yoyote lazima uchanganye ahadi,ubora na picha.

Ahadi hutolewa na Slogan au meme ya biashara, hivyo meme yako inamaana kubwa sana katika kuisimamisha biashara yako mfano. Katika magari Ukiwa unaendesha Marcedez Benz hata kama ni ya mwak 1921 bado slogan yake ni "expensive car" hata kama kiuhalisia sio kweli ila kwa vile brand yao ilitoa meme ya hivyo mteja anaweza kwenda kununua sio kwa sababu anaipenda Marcedez hapana ila tu ni kwa sababu its expensive car, gari aina ya BMW ni "comfortable car" nayo pia vivyo hivyo.

Sasa basi nafikiri umepata picha ni kiasi gani meme inaweza kuathiri picha ya biashara yako aidha ukiifanya vibaya au vizuri. Chini hapa nakuwekea muongozo wa kupata meme nzuri.

Motto ni kitu muhimu katika brand na baadhi ya nguzo zake ni
  1. Iwe ya kipekee kama nembo ilivyo
  2. Isiwe ngumu
  3. Iwe fupi inayoeleweka na nyepesi kukumbukwa

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango