Jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia

Habari tena wanabranding, natumai mu wazima bukheri wa afya leo nimeona tukumbushane kidogo baadhi ya vitu ambavyo vitatusaidia wote kwa pamoja kuongeza masoko na kukuza uchumi wa taifa hili.

Mada yetu leo inasema jinsi ya kutafuta masoko kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia siku baada ya siku. Utandawazi umebadilisha mambo mengi sana katika maisha ya mwanadamu na miongoni mwa vitu ambavyo viliguswa ni pamoja na sekta ya biashara ambapo kadri mambo na siku zinavyoenda nayo inaenda inabadilika hasa kwa huku kwetu nchi zinazoendelea.

Teknolojia imekuja kurahisisha baadhi ya kazi na utendaji kazi wa eneo fulani miaka ya nyuma ilikuwa kama unahitaji kusajili kampuni yako ni lazima uende Brela ukaandike jina, utume barua, wakujibu ndio uanze kuomba usajili lakini sasa hivi kila kitu unakifanyia nyumbani kwa kutumia kompyuta yako tu. Tra nao vivyo hivyo ilikuwa ni lazima uende ofisi zao ili kulipa kodi lakini sasa unaweza kutuma hata kwa simu, hayo ni baadhi ya mabadiliko ya teknolojia kulingana na wakati

Lakini leo nitaongelea kwa upande wa masoko, teknolojia imeathiri pia hata katika upande wa masoko zamani ili ujitangaze ilikuwa ni lazima utumie ama Redio,Televisheni,Gazeti,Vipeperushi na Mabango lakini kwa sasa kulingana na ukuaji wa teknolojia na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao sasa sehemu nzuri ya kujitangaza na kutangaza biashara yako ni kwenye mitandao,zamani makampuni yalikuwa yanaweka bajeti kubwa kwa ajili ya kujitangaza kupitia offline media lakini kwa sasa mitandao ndio ambayo inapokea na kutangaza makampuni na biashara nyingi kuliko zote,japo njia za zamani haziwezi kupuuzwa lakini sasa hivi jitahidi sana unakuwa na vifuatavyo

1. Akaunti katika mitandao ya kijamii
2. Tovuti
3. Blogu
4.Podcast
5. Barua pepe.

Hali inazidi kubadilika hatujui teknolojia italeta nini kesho lakini mambo yote yanahamishiwa katika mitandao hivyo jitahidi kwenda na soko ili upate mauzo zaidi na hii imechangiwa na gharama,kujitangaza kupitia mtandao gharama yake iko chini kulinganisha na kujitangaza kupitia njia nyingine.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango