Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 4)

4. Tengeneza vipengele 3 vya  brand vilivyobaki.

Baada kuziangalia zile  hatua 3 hapo nyuma ukishazipitia zote sasa unaingia katika kutengeneza vipengele  3 vya brand vilivyosalia ambavyo ni Brand ya mtu, Brand ya bidhaa na brand ya mfumo.ili kuikamilisha Brand nzima kwa ufasaha ni lazima uwe umejitosheleza katika vipengele vyote vya Branding.

sasa basi Brand ya mtu inawakilisha muonekano wako na jinsi unavyowahudumia wateja ambapo kila kitu unachokifanya unatakiwa utambue kinapokelewa kama ujumbe katika masikio na maisha ya watu,hivyo ni lazima wewe  mwenyewe ujibrand kufikisha ujumbe sawasawa na ahadi ya brand yako, kama brand inasema usafi na wewe ni lazima uwe msafi na kama brand inasema huduma bora ni lazima huduma bora ionekane kwako bidhaa haileti hivyo vyote,japo bidhaa ndio inakuwa na muonekano wa kumvutia lakini haiwezi kumuongelesha hivyo mteja akipenda lazima atawasiliana na wewe hapo ndipo brand ya mtu inapopata nafasi zaidi.

Brand ya bidhaa hapa ni lazima uhakikishe ahadi unayoitoa katika muonekano wa bidhaa inakuwa sawa na bidhaa yenyewe, kama ahadi uliyomuwekea mteja wako ni bidhaa bora ama huduma bora basi hakikisha bidhaa/huduma yako inakuwa bora kweli kweli ili brand isije kujipinga yenyewe kwa yenyewe.

Kipengele cha mwisho ni brand ya mfumo, hapa mfumo ikiwa namaanisha taratibu za uendeshaji na usimamizi wa brand yenyewe ambapo zinakuwa na pande mbili upande wa ndani yaani taratibu na mfumo wa ndani jinsi ya kufanya brand ionekane na itambulike vizuri na nje ambapo pia kuna taratibu za kimfumo kuifanya brand imfikie mtu husika kwa utaratibu unaotakiwa na kwa uhakika zaidi, pi mteja mwenyewe anapokuja kupata huduma hupenda kupata huduma kwa mfumo, nafasi ya kutoa kazi sehemu ambapo amepokelewa na mtu mwingine akaulizwa shida akapelekwa kwa mhusika mwingine kisha akamalizia kwa mtu mwingine mteja ananafasi kubwa ya kuichagua huduma hiyo kuliko ile ambayo mtu mmoja anafanya kazi zote.

leo nitaishia hapa toleo lijalo nitaelezea hatua ya 5 katika hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo,ili kuendelea kupata machapisho yangu bonyeza kitufe cha (follow) upande wa kushoto chini na kila nitakapotoa uzi utapata taarifa ama kwa wale walioko katika mtandao wa facebook unaweza kulike page yangu Elisha Chuma, Pia unaweza kuungana nami kwa kundi la whatsapp kwa kutuma namba yako kwenda 0684047323.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango