Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 5)

5. Tengeneza brand ya promosheni

Katika kazi zako zote usitake zote zitoke kwa pamoja ni lazima uchague moja ambayo itakutambulisha na ndio utakayoifanyia promosheni na matangazo sana,mara nyingi na imeshazoelekwa kwa nchi za kwetu huku kampuni moja kuwa na biashara zaidi ya moja yaani kuwa na vibali ama kutumia jina moja kufanya biashara ama kutoa huduma kwa kada zaidi ya moja, Mfano utakuta kampuni ni Nyarubamba Company na inahusika na Ushauri wa kifedha,usaili, na huduma za kibenki,hapo sasa kampuni ni moja lakini inafanya kazi 3 kwa wakati mmoja,sasa basi katika ulimwengu wa biashara kila tawi la hizo biashara ni biashara kamili hivyo ushauri wa kifedha ni biashara kamili, Usaili ni biashara kamili na pia huduma za kifedha ni biashara kamili kwa muonekano ni kama vile zote ziko kwenye mlengo mmoja wa fedha lakini zinatofautiana utendaji wake wa kazi, sasa basi unachotakiwa kufanya ni lazima uchague tawi moja ambalo utakuwa unalifanyia promosheni na sio yote, yaani unatakiwa kuchagua kama ni Ushauri wa kifedha ama usaili, au huduma za kibenki kimoja wapo ndio ukifanyie promosheni hii itakusaidia kuijenga brand katika mlengo sahihi ambapo brand ikiendelea kukua na kusimama ndipo unaweza kuanza kubadilisha nguvu katika aina za matawi yako.

Mfano: Mitandao ya simu hutengeneza bidhaa nyingi nyingi lakini kila bidhaa hupewa muda wa kufanyiwa promosheni hadi izoeleke na iwe ndani ya vichwa vya mteja wanaomtarajia, sasa hapa usije kujilinganisha na wenye mitandao ya simu sababu hata wao pia wanaushindani na sio wote wanafahamika ama wananafasi ya kutosha katika soko, kuna mitandao mingine ambayo haijafanikiwa japo ipo inafanya kazi, hivyo unatakiwa kutambua aina ipi ya kazi zako ambayo utaifanyia promosheni kwanza kabla ya nyingine ili kuikuza na kutengeneza utambuzi kwa wateja wako.



leo nitaishia hapa toleo lijalo nitaelezea hatua ya 6 katika hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo,ili kuendelea kupata machapisho yangu bonyeza kitufe cha (follow) upande wa kushoto chini na kila nitakapotoa uzi utapata taarifa ama kwa wale walioko katika mtandao wa facebook unaweza kulike page yangu Elisha Chuma, Pia unaweza kuungana nami kwa kundi la whatsapp kwa kutuma namba yako kwenda 0684047323.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango