Aina za malengo na mipango

Aina za Malengo na mipango

Katika maisha ya kila siku kila mtu hutengeneza malengo na mipango ya kufikia kilele fulani,lakini kutokana na kutokuwa na aina kamili ama sahihi za malengo na mipango watu wengi hujikuta malengo na mipango yao inafeli kwa sababu hujiandaa kwa vitu vichache kuliko uhalisia wenyewe.

asilimia kubwa ya watu hutengeneza mipango bila malengo na matokeo yake ile mipango hufeli sababu hakuna malengo kamili,katika maisha ya kila siku kuna mipango ya aina 2 (mbili) na katika malengo kuna malengo ya aina 7 (saba).

hivyo unapofikiria kutengeneza mipango na malengo yako ili ukue na kufikia kile unachokihitaji ni lazima malengo yote yakamilike ndio mipango itafanikiwa kwa ufasaha.

Aina za Mipango - hizi sio aina ngeni kabisa kwa watu japo wengi hawajui kuzitumia na kuitofautisha,kuna mipango aina 2,mipango ya muda mrefu na mipango ya muda mfupi,ili ufanikiwe unatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu ambayo itakuwa ndio imebeba lengo kuu kwa vile safari ya kufikia lengo kuu sio rahisi unatakiwa kuwa na mipango ya muda mfupi ambayo itakusaidia kutokutoka kwenye ramani yako na kuendelea kukua kidogo kidogo kulifikia mpango wako wa muda mrefu.

Aina za Malengo - haya pia sio mageni kwenye masikio yetu lakini wengi wetu huwa tunapanga kwa malengo machache na kusahau mengine matokeo yake tunajikuta yale ambayo hatukuyawekea mipango yanafeli na kuturudisha nyuma malengo yote mengine tuliyoyaanzisha mfano mtu analengo la kwenda mjini na kurudi nyumbani lakini katika mpango wake haweki gharama za chakula na maji matokeo yake akiwa mjini atakula na kunywa mwisho wa siku anajikuta yuko nje ya mipango na kaharibu lengo,na ikifika hapo ndio ule msemo wa "fedha nnapata ila sijui huwa zinaenda wapi"unatokeo sababu unazitumia kwa tumizi la msingi lakini hukuliweka kwenye malengo yako hivyo unakuwa hujioni kama umetumia fedha zako vibaya ila zimekwisha linakujia swali na sijui zimeenda wapi. Unapofikiria kukua ama kuhama kutoka hatua moja hadi nyingine fikiria kutengeneza malengo ya ; KIROHO,FAMILIA,FEDHA,BINAFSI,KIMWILI/KIAFYA,KAZI,KIJAMII haya ni malengo 7 ambayo ukiweza kuyapanga vyema yote basi safari yako ya mafanikio itaanza kuwa na mwanga tofauti na ilivyo sasa.

Kwa huduma ya ushauri na kutengeneza nyaraka za kibiashara,wasiliana nami kwa namba 0713603699


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.