Jifunze kupokea matatizo kama changamoto

Jifunze kuwa mjasiriamali mzuri,ukiyabadilisha mazingira na unayoyaita matatizo kuwa changamoto,utaanza kuziona fursa kupitia changamoto yako,badilisha aina ya mawazo yako usiishi ndani ya boksi la uwezo na uelewa wako toka nje ya boksi lako utaona vitu katika hali ya tofauti sana.

Mfano mdogo ni masikini siku zote anaomba majaribu ama matatizo yasimpate ili aendelee kusimamia eneo lake,lakini anaefanikiwa anatamani changamoto za kiwango cha juu ili atatue na kupanda kiwango,hali hii inakuja hata kwenye nyumba za ibada wanaojihisi hawana wanawaachia michango wanaohisi wanacho mwisho wa siku aliekuwa nacho anaongezewa na asiekuwa anacho ananyang'anywa.

kila kinachopita kwako ni thawabu inategemea na vile unavyokichukulia aidha kitakujenga ama kitakubomoa,chagua kujengwa ili kesho uwe bora zaidi ya jana,hakuna asiekuwa na changamoto ila tofauti ni jinsi ya kuzipokea na kuzifanyia kazi.

Elisha Chuma Snr
www.elishachuma.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango