Kwanini 40 ?


Elisha Chuma
Kwanini vitu vinaangukia siku ya 40
Muda na wakati unatupa mkono sana katika kuijua kweli na hii inasababishwa na vitu vingi mabadiliko ya uchumi,hali ya hewa,mitindo ya maisha,kuiga na vichocheo vingi vinatufanya tunabadilisha ile kweli kuwa kawaida, leo nitaongelea suala la kwanini mtoto anapozaliwa anatakiwa kuwekwa ndani kwa siku 40 ni kitu ambacho tumekikuta tumekirithi lakini tunakiacha, Je vizazi vyetu ama kizazi chako cha 4 kitafahamu kama kulikuwa na kuweka 40 kama kuanzia kwako haujaweka 40?.

Historia,zama na ukweli vinatupeleka mbali sana lakini hii dhana ya 40 haijatumika kwa mtoto tu vipo vingi leo tutaangalia kwanini 40.

Sasa basi katika  ulimwengu war oho kuna kitu kinaitwa Aura hiki kiko kwenye mwili wa hauwezi kukishika wala kukigusa ni kama tabaka lililopo juu ya mwili wako ambalo linakusaidia na kukukinga na nguvu za nje,mfano unaweza kutembea ukahisi mwili umesisimka ghafla tambua hapo aura yako imefanya kazi,ama umepima na unaumwa lakini hujanywa dawa na unajiona mzima tambua aura imekuponyesha vipo vingi kuhusiana na hili nisiende ndani sana,mtoto anapozaliwa aura yake inakuwa haijajitengeneza hivyo zile siku 40 huwa za kuitengeneza aura na kuifanya ikomae iwe na uwezo wa kupambana na nguvu za walimwengu,mzunguko huu hutumia siku 40 ndipo inakuwa imekomaa ukimtoa ama ukimkutanisha na walimwengu kabla ya muda wake inamaana aura yake inaweza kuathirika sababu itajitengeneza tayari ikiwa na madhaifu, mfano: mtoto akiwa mchanga kabla ya siku 40 ukimtoa akakutana na watu wa aina mbalimbali wote hawawezi kuwa sawa kiafya,kiusafi,kimatendo,hata kiimani hivyo ni rahisi kwa mtu anaembeba mwanao kupenyeza ama kumuambukiza kitu ambacho hawezi kukikataa sababu aura yake haijakomaa.

Lakini pia kwa mtu anapofariki vile vile Aura huwa bado imeungana nae na vitu vyake huisha nguvu taratibu taratibu hadi kupotea kabisa siku ya 40,kuna kesi nyingi za watu kutumia vitu vya marehemu kabla ya siku 40 na wakawa wanamhisi marehemu kwenye vitu vyake,hapo sio hisia za kimawazo inakuwa ni aura inakuunganisha na  roho ya marehemu hivyo anauwezo wa kuwasiliana nae kihisia lakini kwa vile hautambui lugha ya rohoni unaweza kuhisi mauza uza,ndio maana hata kugawana vitu huwa ni baada ya siku 40 ambapo inakuwa tayari aura ya marehemu imeachana na vitu na kuambatana na roho yake.

Kwa upande wa kiimani 40 inamaanisha “ukomavu” hivyo hata kwenye biblia Yesu alipofunga siku 40 ilikuwa ni ukomavu wa kuanza kazi ambayo alikuja kuitimiliza,vivyo hivyo kwa Musa ilikuwa ni ishara ya kuonyesha ukomavu kwa jambo linalofuata mbele yako  kiimani, kwa wana wa Israel wao iliwabidi miaka 40 sababu ya kufikisha Kaanan kizazi chenye kumtii Zaidi Mungu kumtambua Mungu wa baba zao ambae amewavusha katika matatizo mengi hata pale ambapo kibinadamu waliona imefika mwisho aliwapigania,lakini pia ilikuwa ni ukamilifu wa kufikisha jeshi lenye nguvu Zaidi na wenye uwezo wa kupambana na maadui ikitokea vita hivyo ili ukamilifu wa ahadi utimie ilibidi kizazi cha Musa kiondoke ili iingie damu changa yenye ari na morali ya kufikisha na kukamilisha lengo.

Kupitia ukamilifu huo ndio ikaja na misemo mingine kama siku za mwizi 40,ikiwa inamaanisha siku yako ya 40 ndio ya ukamilifu wako utapatikana tu zile 39 utaweza kukimbia ila siku ya ukamilifu wako ikifika ndio 40 yako,Life starts at 40,Menopouse n.k vyote ni kuonyesha ukamilifu tu wa mwanadamu hata kiakili kimawazo na matendo akifika miaka 40 automatic vitu vinabadilika ndani yake na nje ikiwa tu ni utimilifu wa 40.

Hii ndio maana ya namba 40 “kamilifu”

Chini hapa ni kwa wazazi na walezi tukumbushane kwa watoto wetu,utandawazi unatutawala sana tunasahau asili na misingi iliyowekwa.

Sasa wazazi wa siku hizi akimaliza tu kujifungua mtoto yuko kwenye mtandao,tambua ile ni nafsi changa bado haijawa ana uwezo wa kupambana kabla ya kukomaa tayari unaipeleka kwenye mapambano na kuna nguvu nyingi zisizo onekana zinazotafuta nafsi changa kuziharibu, unaweza kutoa nafasi ya kuharibu maisha yote ya mwanao kwa picha moja uliopandisha akiwa mchanga sababu ya mahaba yako na ulimwengu kutambua kama umejifungua,mtoto anaweza kupandikizwa magonjwa aura inakua na magonjwa ambayo sio ya asili ama kupandikizwa kusudi lisilokuwa la kwake mtoto anakuwa tofauti kabisa na matarajio kila siku unalalamika afya yake mbovu kumbe imeletwa na kuiruhusu dunia kukutana na mtoto akiwa bado hajakomaa.

Hakuna mzazi aisiependa mwanae hivyo siwezi kuwakumbusha kuwapenda,ila tukumbuke sio kila tamaduni tunazoziiga zinamanufaa na zina madhara ya moja kwa moja madhara yanaweza kuwa yasiyoonekana mara moja akakua nayo na ukayazoea ukahisi ndivyo alivyo kumbe sababu ilikuwa ni kosa la mwanzo. tulizingatie hili siku 40 sio nyingi mpe nafasi mwanao kuwa na afya,nguvu,akili,upeo na kusudi imara aliloandaliwa.MPENDE ZAIDI MWANAO WALIMWENGU WAPO TU.

Elisha Chuma.

Instagram:@elishachuma

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango