Namna bora ya kujitangaza

Soko limebadilika sana kulinganisha na zamani watu wengi sasa hivi wameanza kutambua umuhimu wa kjitangaza na biashara nyingi sasa zinafanya branding(Chapa), kwa ajili ya kupata nafasi katika soko husika, lakini tunashida moja, hatujaweza kuwatumia washauri wa mambo ya biashara ipasavyo, tunapungua sana.
Watu wengi wamekuwa na shida kuhusiana na jinsi ama namna bora ya kujitangaza sababu ya kutokutambua ni lini utangazaze, saa ngapi ? na nani anaetakiwa kuona na sio hivyo tu bali hata kwa njia gani. 

Hali hii inachangiwa kwa namna moja ama nyingine na mfumo wa biashara lakini pia kuna visababishi kama
soko la utangazaji kukosa watu wengi wenye weledi wa jinsi ya kujitangaza lakini wateja kuwa na maamuzi zaidi ya kile ambacho soko linahitaji pia matumizi ya wataalam na watoa ushauri kwa habari ya biashara na branding.

Biashara nyingi zimejikuta zinafeli si kwasababu hazina bidhaa nzuri hapana ni kwa sababu hazijitangazi vizuri, sasa kuepuka hayo fuatana nami ili utambue vitu vya kufanya.
Leo tutapitia vichache vya msingi kuangalia unapotaka kujitangaza.
  1. Namna bora ya kujitangaza
  2. Tangazo lako linatakiwa liweje
  3. Muda gani mzuri wa kujitangaza
  4. Nini kisikosekane
  5. Muda gani mzuri wa kujitangaza
Namna bora ya kujitangaza inatengenezwa na :-
  1. Kujitangaza kwa kufuata soko lako
  2. Kujitangaza kwa weledi na mbinu mpya
  3. Kujitangaza kwa kufuata misingi ya utangazi kulingana na wakati husika
  4. Kujitangaza kwa kumlenga mteja wako.
Tangazo lako liweje.
  1. Kwanza kabla ya kudili na tangazo unatakiwa ujue mteja wako ni nani? Anataka nini?,anataka kusikia nini? Na kupitia wapi?
  2. Tangazo lako siku zote linatakiwa liwe na muonekano wa hadhi yako
  3. Liwe na uhalisia wa unachokifanya
  4. Ni lazima ucahgue wewe ni nani kati ya watatu ambao mteja wako anachagua 1. Mkufunzi
    2.Uzoefu 3.Mshauri, mteja wako siku zote anahitaji kufanya kazi na mmoja kati ya hao haijalishi ni
    unafanya biashara gani.
  5. Tangazo lako hakikisha halina kelele,yaani vitu vingi bila mpangilio na kumbuka kila sekta ina aina
    yake ya kujitangaza na kuna sekta ambazo haziruhusii kabisa kujitangaza.
  6. Unapojitangaza ni lazima ufate Sekta,Mteja na trend.

7. Vitu vinatofautiana kulingana na aina ya tangazo lako baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na businesscards,Flyers,Posters,Brochures,Online adds,Banner, Tshirt na vingine vingi tunaviita kwa pamoja Promotional material. Vyote hivi vina aina na jinsi ambavyo vinatakiwa vitumike na kutengenezwa usichanganye kwa kufuata mihemko.

Nini kisikosekane kwenye tangazo lako
  •   Tangazo lako ni wasifu hivyo vitu vya muhimu ni pamoja na
  •   Mawasiliano (unapopatikana,mitandao n.k)
  •   Lengo Kuu
  •   Jina


    • Muda gani Mzuri wa kujitangaza
  1. Muda mzuri wa kujitangaza ni pale ambapo hali ya ushindani upo juu
  2. Pale ambapo kila bidhaa inajitangaza
  3. Muda ambapo unahitaji kutengeneza muonekano wako
  4. Muda as wakati inategemea na aina ya biashara na mbinu ambazo unatumia kuna biashara
    ambazo zinafanya matangazo kabla hata ya kuanza na kuna nyingine baada hii yote ni jinsi
    ambavyo brand yako unataka iwe
  5. Hivyo vyote na vingine vinasimamiwa na branding plan hivyo hata kutambua muda wa
    kujitangaza ukiwa na plan ni rahisi sababu kila biashara inatumia mbinu zake.
  6. Mhimili wa mauzo yako ni matangazo usikimbilie kwenye bidhaa kwanza bila kufikiria matangazo
    sababu mteja wako haanzi na bidhaa ila tangazo.
Kujitangaza kuna aina 3

Media ,Online na Offline zamani kulikuwa na offline,mini media na max media,sasa hivi ni wewe kuamua tu unafuata njia ipi offline,online ama media ,japo soko liko online kw sasa.
Kuna watu wanaotumia mitandao kujitangaza , na hawafanyi branding soko linabadilika kila siku zamani ilikuwa sawa tu kwa kufanya unavyojiskia lakini sasa hivi mambo yamebadilika watu/ wateja wanahitaji brands, utakuta picha imepigwa inawekwa namba kisha wanasema ni tangazo. Kila kitu kinamisingi yake ukifanya kwa kujiskia mwisho wa siku huwa sio mzuri natamani siku moja watu wote waelewe madhara ya kufanya hivi na wabadilike lakini elimu huchukua muda.kuwafikia walengwa na wahusika kuikubali. 


Elisha Chuma
Mshauri na Muelimishaji
+255 745 10 80 10

(Namna bora ya kujitangaza)
Namna bora ya kujitangaza na kupata wateja

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango