Hatua za kufuata unapofikiria kuanza kufanya biashara yoyote


Watu tumezoea kudanganyana na kutokuelezana ukweli kuhusiana na biashara, tumekuwa watu wa kupeana moyo na kushauriana kila mtu afanye biashara lakini biashara au ujasiriamali sio kitu rahisi kiasi hicho ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu. Hivyo usijitumbukize tu katika bishara kwa kufuata mkumbo aidha umeambiwa biashara fulani unaiweza, biashara fulani inalipa au wewe unaweza kufanya biashara fulani na ikakulipa, kila kitu kinaugumu wake na changamoto zake, changamoto za muuza maandazi ni tofauti na changamoto za muuza duka,hata ujuzi wa msusi ni tofauti na wa kinyozi japo wote wapo saluni,hivyo unapoamua kufanya biashara fulani usikurupuke fikiria na tathmini kwanza kwa undani kama inaendana na wewe zifuatazo ni baadhi ya njia au mbinu muongozo za kufuata unapotaka kuanza biashara yako.
  1. Wazo la biashara.
    Kitu cha kwanza unachotakiwa utafute ni wazo la biashara,hii itategemea na eneo pamoja na asili ya kazi yako (kwa muongozo wa jinsi ya kupata wazo la biashara.jinsi ya kupata wao la biashara),hakikisha wazo ulilolipata linaweza kukupa mafanikio, usitumie wazo la kujaribu kuna watu hufanya biashara kwa kujaribu yaani anafanya kuijaribu biashara kama itamlipa, ukifanya biashara kwa mtindo huo haiwezi ikakulipa na haiwezi kukua mafanikio yake yatakuwa hafifu sana.
  2. Utafiti wa kwanza
    Baada ya kuchagua wazo bora la biashara usikurupuke kuanza kwa sababu umepata wazo zuri na bora la biashara basi ndio unaanza mara moja,hapana mara nyingi unapotengeneza wazo huwa unatengenezea na faida hivyo ukiwa na wazo faida ni nyingi kuliko matumizi hivyo usikurupuke kitu kinachofuatia na kuanza kutafiti, fanya utafiti kama kuna mtu au sehemu nyingine kuna biashara kama unayoitaka kuifanya nenda fanya utafiti kwa kupitia biashara yake, ongea nae akueleze ni changamoto gani anapata,kiwango cha faida,hasara,gharama,ugumu na pia mbinu zake,kama hakuna mtu anaefanya biashara kama hiyo anza kufanya utafiti kupitia mtu wa mwisho kupokea bidhaa yako, utafiti wa
    1. Bajeti = Fanya utafiti wa bajeti yako unatakiwa iweje ili ukamilishe na kuifanya biashara yako ianze na
      afya.
    2. Muda = Fanya utafiti wa muda, ni muda gani utatumika kuanzia katika utafiti wako wa
      kazi hadi kufikia
      katika mafanikio yako.

    3. Nguvu kazi = Fanya utafiti wa aina na uwezo wa nguvu kazi inayohitajika katika biashara yako ili pia
      utengeneze na mfumo mzuri wa hiyo biashara.
    4. Vifaa = Fanya utafiti wa vifaa vitakavyotumika gharama zake, uwezo wake na uimara
      ili ujue ni kifaa
      kipi kitakufaa na kipi hakitakufaa.

    5. Faida = Fanya utafiti wa faida yake,kulingana na uhitaji wa wateja watarajiwa hii itakupa muelekeo
      wa biashara yako kama italipa mapema au itachukua muda, kama itakugharimu sana au
      itaanza kujihudumia mapema.
    6. Washindani = Fanya utafiti wa washindani wako pia wa aina zote tatu na uione nafasi
      yako kwao je?
      ukianza biashara utakuwa tone la maji baharini au mafuta kwenye

      maji,angalia mbinu zao uwezo wao na mapingufu yao.
g. Eneo = Eneo litakalofaa kwa aina ya biashara yako na mbinu zako
  1. Mpango biashara
    Baada ya kufanya utafiti huo utakupa mwanga wa ni kitu gani kinahitajika na nguvu kiasi gani itakuweka usimame unapopahitaji,sasa kinachofuata ni kutengeneza mpango biashara ( Business plan) ambayo ndiyo itakuwa kama muongozo wako kwa kipindi husika,baadhi ya vitu utakavyoainisha na kuvifafanua katika mpango biashara wako ni pamoja na .
    1. Utafanyaje = Hii ikiwa inamaanisha utendeji wako wa kazi utakuwaje na utaupeleka namna gani
    2. Muda =Utaonyesha muda wa kuifanya hiyo kazi na jinsi itakavyofanyika
    3. Mbinu = Kwa vile umeshatambua washindani wako na umeshatambua udhaifu wao
      tengeneza mbinu
      ambazo zitakuwa haziwaakisi moja kwa moja washindani wako ila

      zinawaathiri baada ya muda.
    4. Washindani = Orodhesha washindani wako na uandike mbinu utakazotumia kupambana nao,
    5. Mipango = Tengeneza mipango ya biashara yako ambayo utaifanyia kazi ili kufikia mpango mkubwa
      mipango hiyo iangalie uwezo na kasi ya biashara ili isije kuwa juu au chini ya kiwango cha
      biashara yako kuna mipango ya muda mrefu na muda mfupi,Fanyia mipango yote.
  2. Utafiti wa 2
    Baada ya kutengeneza mpango biashara yako sasa fanya utafiti mdogo wa mpango biashara yako kama ukiiweka sokoni italeta mafanikio au haitaleta mafanikio,kwenye ulimwengu wa biashara kuna tofauti kubwa kati ya mawazo na kitu/hali halisia

Ukiona unanafasi katika biashara hiyo basi fanya na anza mara moja kwa kufuata muongozo wako ulioutengeneza hapo awali,kama unaona nguvu yako ni ndogo kulingana na soko na ulivyojipanga,badilisha mpango uendane na soko pamoja na uwezo wako.


Nukuu: Uwezo na nguvu ni akili,fedha ni mwezeshaji tu
Kuna tofauti kubwa kati ya wazo na kitu halisi jitahidi kusimamia na kufanya ulichokiwaza
mwanzo
Ujasiriamali na biashara sio kitu cha kujaribu.AMUA fanya,jaribu ACHA



Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango