Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme

Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme.

Watu wengi kwenye mahusiano huchanganya kipi kinahitajika wapi na kipi kinawekwa wapi,ugomvi na kutokuelewana vinachukua sana nafasi sababu kila mtu hajui anakosea wapi na anajiona yuko sahihi.

Iko hivi utambue leo.
Mwanaume maisha yake yote hahitaji kupendwa,uhitaji wake mkubwa kwenye mahusiano sio kuonyeshwa anapendwa ama kufanyiwa vitu vya kudhihirisha upendo wako,atavichukulia kawaida wakati wewe umevichukulia pakubwa sana na utalalamika hupendwi,kumbe umemkosea hitaji la mwanaume kwenye mahusiano ni "Heshima" mwanaume anahitaji kuheshimiwa tu,ukimuheshimu kwake ni tafsiri ya unampenda ndio maana ili kumlegeza mwanamme na kukupa unachotaka mwanamke akishusha sauti na akaongea kwa upole,ustaarabu na utii mwanaume hufanya kile mwanamke anachokitaka sababu ameonyesha heshima,hivyo mwanamke usipambane kuonyesha unampenda ila onyesha unamheshimu.

Lakini hali iko tofauti pia kwa mwanamke yeye anapenda kwa hisia na kudhahania,ukizijali hisia zake na kuzipenda utakuwa umemaliza kila kitu,ndio maana mwanamke anaridhika na anapata furaha hata kwa zawadi ya pipi tu ya Tshs.100 kwake inamaana sana sababu umeonyesha kuzijali hisia zake na umemkumbuka,umempa wakati wako kumuwazia na hadi kumnunulia zawadi,hajali sana aina ya zawadi ila msukumo wa hisia zako hadi kumletea ama kumpa zawadi.

Kwenye biblia  hivi vitu viko wazi

wakolosai 3 : 18 - 19 (Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. KOL. 3:18‭-‬19 SUV)

Hii inamaanisha kwa kuanishwa udhaifu wa kila jinsia,mwanamke tatizo lake ni kutii na mwanaume tatizo lake ni kupenda,ili kufikia kuwa mwili mmoja lazima kiwepo kipindi cha kupokea madhaifu ya mwenzi wako uone kama utaweza kuishi nayo kipindi hiki kinaitwa uchumba na mkiona kila mtu anaweza kuyabeba madhaifu ya mwenzake basi ndio hatua ya ndoa hufikiwa.

Tatizo kubwa kwa kizazi cha sasa ni wanawake wanaonyesha upendo badala ya heshima na upendo wake usipowekewa hisia sawa na alizoweka yeye anahisi hapendwi na mwanaume badala ya kuonyesha upendo na kupenda anaonyesha utii matokeo yake anajikuta kwenye mzani wa nani anamtii mwenzake zaidi...kuwa kwenye mahusiano na kuachana mzunguko wake ni mmoja.

Ili mwanamke akupende akukubali kwanza ni anatumia hisia na imagination zake kuhusu wewe na mazuri na jinsi atakavyokuwa kwenye uhusiano,ambapo mwanaume anapomuona mwanamke huwa inawaka tamaa hivyo huelezea tamaa zake iwapo mwanamke atakubaliana na maelezo ya tamaa za mwanaume basi huanza kuonyesha heshima kwa huyu mwanaume humpa nafasi tofauti na wengine ilu kuona kama zile hisia na vitu alivyotegemea vitakuja,ambapo kwa mwanaume akipewa nafasi zaidi yeye huona ndio anapendwa huanza kuonyesha upendo kwa kuzijali hisia,kumjali na kumpa muda kama anavyoutoa ikiwa hali itaendelea hivi basi mahusiano yatadumu kwa kipindi kirefu .

Lakini ili kuachana pia ni mwanaume hupunguza kiwango cha kuonyesha upendo aidha ni kwa sababu ya mazoea,malumbano ama sababu nyingine na ili kiwango kipungue lazima mwanamke atakuwa amepunguza utii kwa huyu mwanaume kwahiyo mzunguko unakuja kuwa mwanamke anasubiri hisia na upendo kutoka kwa mwanamme anakosa anaamua kupunguza kidogo kasi ili mwanaume agundue kuna kitu kinapungua,mwanaume badala ya kuona upungufu yeye huona hapendwi hivyo na yeye kwa vile hapendwi atapunguza kuonyesha anapenda na kujali hali itaenda hivyo hivyo kwa kila mtu kupunguza hisia mwisho mahusiano yanabaki jina ila hisia hazipo tena na matokeo huwa ni kuachana..na kwa wengine hatua hii hufika mapema hata kabla hisia hazijaisha na kibaya huwa kila mtu anajihisi yuko sawa.

Mwanamke kamwe usimchukulie mwanamme kama mwanamke alievaa suruali usimtreat kama shoga yako wa kike pia mwanamme usimtreat mwanamke kama mshkaji ako wa kiume,kila mmoja anamtegemea mwenzake.


Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango