Jiandae kufeli

Biashara,Mahusiano,Mipango mingi inafeli sababu watu hawajiandai na changamoto za anachokitafuta ama kukifanya matokeo yake anawaza faida tu,zinapokuja changamoto zake anajikuta anafeli kirahisi sana

Biashara nyingi zinapoandaliwa huwa ni kw mpango wa "high season" mauzo yako juu lakini uhalisia hakuna biashara ambayo inakuwa kwenye high season mwaka mzima ni lazima kuwe na kipindi cha "low season" mauzo hafifu na hapo ndio biashara nyingi hufa,kwa kuwa hazikujiandaa na low season matokeo yake ni kula mtaji na kupumzika,hili ni janga la biashara nyingi...UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WAZA NA KIPINDI CHA KUFELI AMA KUPOROMOKA KWA BIASHARA UTAFANYA NINI?.

Kwenye mahusiano wapenzi wengi huingia wakitegemea raha tu na furaha na mara nyingi mwanzo wa mahusiano kila mtu hujitahidi kufanya ili kumridhisha mwenzake,ila baada ya muda ile hali ya kuridhishana huisha huingia hali ya uhalisia hapo ndio shida huanza,vikwazo,wivu,husda,vijitabia huonekana,sasa kwa kuwa akili ya wengi huwa ni mpenzi wako ni furaha yako 100% hujikuta wanaumia sana na kufeli kuendelea ama hata kutengeneza magonjwa ya hisia..ILI UDUMU NA UISHI VIZURI KWENYE MAHUSIANO ONDOA HALI YA UMILIKI NA WEKA HALI YA URAFIKI,MCHUKULIE MPENZI WAKO KAMA RAFIKI YAKO,HATA AKIKUUDHI UTAWEZA MSAMEHE NA KUENDELEA KAMA UNAVYOFANYA KWA RAFIKI YAKO.

Mipango mingi inafeli sababu watu hawafikirii upande wa pili wa mpango iwapo utafeli itakuwaje,pale inapotokea imeenda kinyume na matarajio watu hughafirika na wengine hutengeneza magonjwa(Mshtuko wa moyo,presha n.k)....UNAPOTENGENEZA MPANGO WAKO WOWOTE WEKA NA ASILIMIA ZA KUFELI NA IWAPO UKIFELI WEWE UTAFANYA NINI AMA KUWA KWENYE HALI GANI?.


Maisha ni haya haya,wakubadilika ni wewe,wazazi wafundisheni watoto maisha sio kushinda tu kuna kufeli ambako ni sehemu kubwa ya kujifunza,ili waweze kukabiliana na hali za kufeli,kukataliwa,kudharauliwa,kubezwa katika maisha yao.


Elisha Chuma
Mwalimu & Mshauri Maisha,Ujasiriamali biashara na Uchumi.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango