Mafanikio na gharama zake.

Nimekuwa nikikutana na kujadiliana na watu wengi sana kuhusu mbinu na jinsi ya kufanikiwa,nimegundua watu wengi wanayapenda sana mafanikio na wanatamani kufanikiwa lakini hawakotayari kuzibeba gharama za mafanikio hayo.

Kufinikiwa ni kupiga hatua na hakuna hatua inayopigwa bila kutumia nguvu,hata hatua ya mguu wako ili unyanyuke unahitaji nguvu,balance,uelekeo na mambo kadha iko hivyo pia kwenye mafanikio.

Ili ufanikiwe lazima uzikubali gharama za eneo lako la mafanikio,usiwe kwenye kundi la kutamani kila siku na ku"wish" jitoe kwenye hiyo hali kwa kubadilisha mawazo yako.

Na ili ufanikiwe utakavyo tumia gharama kutengeneza mafanikio yako,usiombe kila kitu wakati wewe unatengenezewa kitu.


Mafanikio yanaanza na mabadiliko ya tabia na mtazamo,anza kufanikiwa ndani yako sasa ili uyatengeneze mafanikio ya nje.

Elisha Chuma.
Mwalimu,Mshauri & Kocha wa Mafanikio 

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango