Makosa yanayofanywa na wanaotoa elimu ya ujasiriamali


Kuna kitu ambacho wananchi wanakuwa wanapotea bila kujua kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaohamasisha na kutoa elimu kuhusu ujasiriamali, Sio wote

Watu hao wanawasaidia watu,lakini wanaruka sehemu kubwa ambayo inawaumiza sana
Watu wanaoamua kutumia elimu yao kwa manufaa yao,mfano kuna wale wanaotoa elimu kuhusu
Kutengeneza vitu kama sabuni,shampoo na vinginevyo,hao hutoa tangazo la kuwafundisha watu mbinu
Za kuwa mjasiriamali, wao hufundisha namna ya kutengeneza hadi unaelewa halafu wanakuacha.hilo
Ni kosa kubwa sana kwa wao kumfundisha mtu kutengeneza kitu kinachofanywa na makampuni makubwa kama kazi yao halafu ukamfundisha yeye kwa shilingi elfu 30, bila kujua atatoka hapo atatafuta fedha ya mtaji na mtaji wa kwanza unaweza kuwa ni 50,000 tu hapo ameshapigia hesabu akiuza anauhakika wa kutengeneza fedha nyingi halafu inakuwa tofauti.


Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaoitwa walimu wa ujasiriamali  wanaofundisha mbinu za ujasiriamali siwapingi wala sikidhani nao wanafanya kazi nzuri kuwasaidia watanzia kumeza ilhali hawajatafuna, lakini kuna makosa ambayo nahisi sijuini kutokana na hali ya maisha kutafuta fedha za kujikimu mwenyewe au hawajui bado sijatambua ni kwanini, wanafanya kazi nzuri lakini inamakosa makubwa,kupokea elimu ya ujasiriamali  ni kitu cha busara na neema sana lakini kuitumia hiyo elimu ya ujasiriamali ni kazi ngumu kuliko hata kuipata.

Tatizo linalotokea ni kwamba watu baada ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali , waelimishaji huishia katika eneo la kutengeneza au kufanya ujasiriamali tu ,hakuna kufanya utafiti kama unaowafundisha ni wajasiriamali au wafanya biashara ( kupata maelezo zaidi katika tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali fuatilia matoleo ya nyuma) hivyo kila mtu hupewa elimu hiyo bila kuwapa mwongozo wa biashara ikoje na soko lake likoje wao huondoka na kuwaacha hivyo hivyo wakiwa na ujuzi wao bila maarifa ya soko. Hili ni tatizo linalowapata wafanyabiashara wadogo waliopata elimu ya ujasiriamali wakijaribu kuangalia njia za kutokea kimaisha wengi wao huishia kuwa maskini zaidi sababu hata kile kidogo alichokuwa nacho hakitalipa kulingana na matarajio yake ( kinachofanyika ni sawa na wewe uwe unachimba madini  halafu bahati siku moja ukapata  almasi chafu ukataka kwenda kuiuza ikiwa chafu vilevile kufika sokoni unataka almasi yako iwe na bei ya juu pia, lakini ukakuta sokoni kuna wenye almasi nyingi safi na ukubwa kama wako na wanaziuza kwa bei sawa au chini ya ile bei ya kwako. Kama mteja utanunua almasi safi na kama muuzaji alamsi yako haitauzika sababu haina kiwango, ndio sawa na inavyowatokea wafanyabiashara hawa .wao hufundishwa kufanya ujasiriamali baada ya kufundishwa huachwa ili waitumie elimu ile bila kutambua kama elimu waliyopewa ni kipande tu wanatakiwa watafute au wapewe kitu kizima hukimbila kuanza kufanya biashara huku  wakiwa hawajui kama sokoni bidhaa kama hiyo tayari ipo mwisho wake kwa kuwa hawajajipanga watakuta bidhaa zao haziuziki au hazikidhi malengo kutokana  na ubora au hata jina tu , ukiangalia kwa juu juu unaweza kusema kosa ni la mjasiriamali mwenyewe lakini kosa ni la mfundishaje ujasiriamali ndio aliempotosha kwanza

  1. Hali ya maisha ya wafundishwaji
Kutokana na hali ya ugumu wa maisha wafundishaji hawa hufanya semina zao kwenye wilaya na na vijijini ili kupata watu wengi na pia hutoa elimu hiyo kwa kiwango kidogo cha pesa ili wapate watu wengi. Asilimia kubwa ya watu ambao hujitokeza ni wale wenye kipato cha chini na wengi wao huhisi elimu hiyo ni mkombozi wa maisha yao.

  1. Namna ya ufundishaji
Wafundishaji hawa hufundisha kwa kutumia nyenzo za kisasa na huwa na kipindi maalum cha kutoa elimu hiyo, hivyo mara nyingi hufatilia zaidi kama kile wanachofundisha kinaeleweka ama la na sio yule wanaemfundisha wamemuandaa au wanammezesha bila kutafuta.

  1. Upatikanaji wa vifaa vya kutumia
Baada ya kutoa elimu hiyo waelimishaji hao huacha namba za simu na maelekezo ya sehemu watakapopata bidhaa au vifaa vya kufanyia kazi na kutolea huduma,asilimia kubwa ya sehemu hizo zinakuwa ni mjini mbali kutoka alipo huyu anaepewa maelekezo.

  1. Makosa.
Kosa linalofanyika kwa watu hawa ni kuwapa elimu ya ujasiriamali peke yake bila kuwapa elimu inayoenda sambamba na ujasiriamali, elimu ya ujasiriamali haitoshi peke yake kumfanya mtu awe mjasiriamali tuko katika dunia ya utandawazi mambo yanatakiwa kuenenda kutokana na soko lilivyo na haitakiwi mfanyabiashara kufanya biashara kwa kujaribu sababu unachojaribu wenzako wanafanya kwa maisha yao.

USHAURI:

Kama waelimishaji ni bora kuongeza kiwango cha ada ya kuipata elimu hiyo lakini wahakikishe wanatoa kifurushi kizima cha ujasiriamali mfano: ukija kunifundisha ujasiriamali wa kutengeneza sabuni ya maji, ukanielekeza na namna ya kupambana na washindani,ukanipa mbinu, ukanielekeza taratibu za kufata  na kufanya ili nipate wateja. Itakuwa  umenisaidia sana sababu nikifanya nafanya huku nnajua ninapambana na watu gani na huku ninajua kabisa naingia kwenye vita sihitaji kuingia bila kujiandaa.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango