Tahadhari kwa wafanyabiashara na wajasiriamali
Taa ya hatari
imeanza kuwaka kwa wafanyabiashara na
wajasiriamali wa Tanzania
Asilimia kubwa ya
wafanyabiashara, ( wakubwa na wadogo) wanafanya biashara
Kienyeji na
kikubahatisha wanafanya biashara kama mchezo wa bahati nasibu kupata
Kukosa lakini siku sio nyingi mambo na hali
itabadilika na kubadili mfumo wote wa kibiashara
Hapa Tanzania.
Kwa kuanza kwa sasa
watanzaia wengi wanapata hamasa na hamu ya kuwa wafanyabiashara
Au wajasiriamali kwa
inspiration kutoka nchi za nje, kutoka kwa wajasiriamali wakubwa , kutoka
Kutoka katika vitabu
vya waandishi wa nje ambao huelezea hali ya biashara au ujasiriamali kwa
Kiwango na uwezo wa
sehemu walipo na kwa mjasiriamali wa
kawaida akisoma au kutumi mbinu zile
Zinaweza msaidia
sababu kwa kipindi hicho vitu alivyovisoma sehemu anakovitumia havijulikani
hivyo
Hata akikosea au
kipatia hakuna atakaetambua,hiyo ndiyo hali iliyokuwepo kwa Tanzania ya zamani
lakini
Kwa sasa hali
inabadilika tena sana .
Pili Kwa sasa
wawekezaji wengi wanashawishika kuingia Tanzania na kuanza kuwekeza na kama
nchi ikiwa
Na makampuni mengi
ya kigeni hata mfumo wa kibiashara lazima utabadilika sababu asilimia kubwa
itakuwa
Ni mfumo mpya wazawa
wengi watafeli kwa kuwa itakuwa wameshatengeneza majina lakini kwa mfumo
tofauti
Ambao wameukopi bila
kutumia sawasawa hivyo watajikuta wanapata hasara kwa kuanza upya na kuanza kutafuta
Sehemu nyingine kwa mfano: Zamani ilikuwa ukienda Tra
kuchukua TIN namba ilikuwa haihitaji sana uwe na sehemu ya
Biashara kama ni ya
biashara, Lakini sasa hivi ili upate TIN ya biashara lazima uwe na sehemu ya
biashara na watakukadilia wao kwanza kulingana na gharama zote ulizotumia na
makisio ya mauzo kwa mwezi, kwanini basi wamefanya hivi hii ni kwa sababu
imeonekana watu wanajichukulia tu TIN bila hata ya kuwa na kazi nazo kwa muda
husika mtu anachukua kwa dhamira ya ikitokea inahitajika nitaitumia, Sanjari na
habari maelezo pia ukitaka kusajili gazeti lazima waone hadi mfano wa gazeti
unalotaka,uthibitisho wa fedha za
kulitoa gazeti angalau mara kumi bila kukosa nakadhalika , Hii ni kwa
sababu watu wanafanya biashara kwa kuona faida ukiona mwenzako anapata faida
katika biashara yake na wewe unataka ufanye bila kujua alianzaje hadi kufikia
kwenye hiyo faida mwisho wake unafeli sababu haujui utaratibu wake Ni kitu
ambacho kitu ambacho kitakuja kutokea baadae hata katika usajili wa biashara na
makampuni itawabidi ili usajiliwe ni lazima ulete (business plan)
wakijiridhisha ndio wanakubali kutoa usajili hii ni kutokana na kuwa na
makampuni mengi yanayoanza na kufeli bila kuwa na mbinu thabiti.
Katika biashara kuna
vitu ambavyo bado tunavichukulia masihara bila kujua maana na umuhimu wake
asilimia kubwa ya wafanyabiashara na wanaotengeneza nembo hawajui umuhimu wa
nembo katika biashara yake ikitokea ukamuuliza kwanini nembo yako iko hivyo
atakujibu ni kwa sababu kila biashara lazima iwe na nembo,baada ya makampuni
mengi ya kigeni kuingia yatatokea mabadiliko hata katika nyanja ya matangazo,
leo angalia matangazo yanayotolewa na KFC halafu linganisha na yale yaliyopo
pembeni yake.biashara inafanyika kienyeji hata wanaojua wanatawaliwa na
wasiojua unakuta signboard ya barabarani tangazo limeandika limejaa vitu
biashara inavyomiliki hadi karaha tangazo limechafuka lakini kwa kuwa ni jina
linalong'aa kwa wasiojua itauza na kupata wateja.
Mabadiliko
yanayokuja yanakuja kwa kasi sana ndio maana sasa hivi hata serikali
imeng'ang'ania lebo za TBS hii ni kwa sababu mabadiliko yameanza kuonekana
zamani ilikuwa kama unajua kutengeneza kitu ilimradi ni cha Tanzania na
kimefungwa vizuri hawakifuatilii lakini sasa hivi baada ya kuwa vingi na hawana
uwezo wa kudhibiti kwa haraka wanatoa matanganzo ya watumiaji kutokutumia kama
hakuna nembo ya Tbs.kila sekta sasa hivi ndi inaamka kuanza kufanya kazi kwa
mtiririko unaotakiwa baada ya kuona kasi ya mabadiliko iko juu na bado tuko
mbali , hatari ni kwamba wafanyabiashara hawalijui hilo na hawana hata habari
nalo leo hii mfate mfanyabiashara au mjasiriamali muulize kuhusu branding
atakwambia anajua ya gari,na hata watoa ushauri wengine ukiwagusia Branding wanakwambia ni kubwa sana
kuifanya kwa Tanzania ni ngumu lakini katika biashara bila kubrand ni sawa na
kutembea usiku huku umefumba macho unaweza ukaipatia njia kwa vile umeizoea au
unaweza kuikosea kwa vile sio kila siku itakuwa vile vile. South Afrika
walileta vurugu na ubaguzi kwa wageni kwa sababu walifanya kazi kienyeji na
wageni wakaja kubadilisha mfumo wakajikuta hawapo katika mfumo huo ,ni kitu
ambacho nakiona kimeshaanza kutokea hata Tanzania kwa wananchi wengi kuanza
kulalamika kukosa kazi na raia wa nchi jirani kupewa kazi, tayari maafa
yameanza kuonekana japo wanaogundua ni wachache.
Ushauri:
Kwa wafanyabiashara
na wajasiriamali bado muda upo kidogo wa
kuweza kubadilisha mfumo kwavile hata
serikali yenyewe bado haijajitengeneza vizuri angalia biashara yako fuatilia Branding
jiangalie uko wapi katika mzunguko wa
branding kisha anza kuenenda na mfumo wa dunia nzima ili mabadiliko yanapofika
yakukute umebadilika tayari,biashara ni mchezo lakini unasheria zake hivyo
unaweza kushinda kwa njia za panya kama anaecheza haujui mchezo ila huwezi
kushinda kwa njia za panya kama unaecheza nae anajua mchezo unatakiwa uchezwe
vipi.
Comments
Post a Comment