Vitu vitano vinavyosimamia biashara yako
Biashara pia inavitu
ambavyo kila mtu anatakiwa avifuatilie ili uweze kuimanage, biashara nyingi
zinafeli iwapo moja kati ya vitu hivyo
vinapopungua au kukosekana hivyo basi kabla ya kuanzisha au kuanza biashara yako
jiaminishe unaweza kusimamia vitu vifuatavyo.
1.Branding
Branding ni
muonekano wa biashara yako kwa mteja unaemkusudia, hii ikiwa inamaanisha lazima
ujue mteja wako anataka akuonea katika hali gani ili akuamini , mteja wako
unataka apate kitu gani kichwani mwake mara tu akiiona alama yako
nakadhalika,kuijua elimu hii kutakusaidia sana katika uendeshaji wa biashara
yako kwa sababu itakuwa ni rahisi kwako kujua saikolojia ya mteja wako na
kuepusha kufanya yasiyo sawa katika biashara
na pia ukiiifahamu branding itakufundisha pia njia za
kupambana na wateja na mbinu za kiushindani.
2.Masoko ( Marketing)
Masoko ni sehemu
ambayo inahitaji umakini mkubwa baada ya kufanya brand ya biashara yako kitu
kinachofuata ni kutengeneza na kutafuta masoko ya brand hiyo kwa kuwa utakuwa
unambinu za kutosha hivyo na ukifahamu vizuri kutafuta masoko biashara yako
itakuwa ni brand inayojitofautisha zingine kwa sababu hata kama kukiwa na watu
wengi waliofanya brand kila mtu atafanya kwa mbinu zake ili asifanane na
mwenzake , hivyo kuijua elimu ya masoko ni jambo la muhimu sana na la msingi
katika biashara yako.
3.Huduma kwa wateja(customer care)
Hili ni janga kubwa
kwa hapa nchini sehemu kubwa na biashara nyingi hazitoi huduma kwa wateja
inayotakiwa na kutokana na kuzoea hivyo imefikia hatua imeonekana ni kawaida
kwa mtoa huduma kwa wateja kuto kukidhi haja za mteja na mteja kuondoka
kajilazimisha kuridhika wewe mwenyewe ni shahidi katika hili,lakini elimu hii
ni ya muhimu sana kwa ukuaji wa biashara yako ili biashara yako ikue katika
kiwango unachokihitaji basi inatakiwa watoa huduma wawe na uelewa mkubwa wa
utoaji huduma kwa wateja ,kugundua saikolojia ya mteja anapoingia tu ndani ya
biashara yako ni faida kubwa kuliko kutomgundua hadi akufanye umgundue.
4.Imani (Believeness)
Imani inasehemu
kubwa sana katika mafanikio ya biashara yako na imani yako inachangia kwa kiasi
kikubwa aidha kupata au kukosa katika mzunguko wa biashara yako,kila mtu
anaimani haijalishi ni ya dini au ya mizimu lakini kila mtu ana imani na imani
hiyo huwa ni kwa Mungu wake ambaye huwa anaamini anauwezo wa kumtendea miujiza
na kumsaidia haijalishi ni yupi, hivyo basi biashara haihitaji mchanyanyiko wa
imani zaidi ya moja ndani yake inahitaji
imani moja tu ambayo itaisimamia siku zote kwa mfano ukiwa unaamini dini
halafu ukaenda kwa mganga kutafuta dawa ya kukuongezea wateja biashara yako
haitafanikiwa lakini ukiwa haumini dini yoyote tofauti na kwa waganga biashara
yako itafanikiwa ndio maana mnaweza wote kwenda kanisani mnaumwa mwenzako
akapokea uponyaji na wewe ukakosa au mnaweza kwenda wote kwa mganga mwenzako
akapandishwa cheo wewe ukabaki hii ni kutokana na imani yako inakuwa pande
mbili Mungu yule yule unaemuomba ili akulinde usiku kucha ndio Mungu yule yule
mwizi anamuomba akuibie bila kudhurika na anakuibia bila kudhurika kwanini ,
hii ni kwa sababu mwizi imani yake iko juu kuliko ya kwako uwezeakano unahirizi
na biblia au Quran kwa wakati mmoja. Hivyo imani yako inanafasi kubwa katika
biashara yako.
5.Sheria za pesa( Money principles)
Kila kitu kinasheria
zake hata kula pia kunasheria zake hivyo hata kwa pesa tunazotumia nazo pia
zinasheria zake ambazo kwa kila mtumiaji anatakiwa azitumie ili aendelee kuwa
nazo na sheria hizo hazijalishi ni kwa mwenye
pesa nyingi au kidogo ndio maana unaweza kukuta mtu anaelipwa mshahara mdogo
anamaendeleo kuliko anaelipwa mshahara mkubwa, hii inamaanisha sheria za pesa
ni za muhimu kufuatwa katika kitu chochote sanjari na biashara pia mfano: Pesa
iko katika mchezo wa kunyang'anyana kama ikitoka kwako inakuja kwangu na kama
ikitoka kwangu basi inakuja kwako, hivyo ili biashara yako ikue na iendelee
lazima iwe ndani ya sheria hizo za pesa.
thanks bro
ReplyDelete