Aina tatu za imani zitakazokurudisha nyuma katika biashara yako
Biashara haiangalii unaamini kupitia nini, biashara haiangalii wewe ni mkristo,mpagani muislamu au mhindu,lakini kuna imani ambazo biashara inakutengenezea na inataka ufanikiwe kupitia hizo, hivyo ilikufanikiwa katika biashara yako unatakiwa upitie ukipishana nazo lazima matokeo yake hayatakuwa mazuri.
1.Naweza kufanya kila kitu mwenyewe.
Hii inakuja pale mtu anapoanza kujiona yeye ni mzuri na
mwelevu wa kila kazi katika biashara yake , lakini ukweli ni hauwezi kufanya
kazi zote , ufagie , uhasibu,afisa utumisishi, afisa rasilimali watu na hata
masoko wewe mwenyewe?
Ukweli ni kwamba
hauwezi ukawa mzuri wa hizo kazi zote ni lazima utakuwa na sehemu yako ambayo
unaweza kufanya vizuri zaidi ya nyingine ,
na kama unataka biashara yako ifanikiwe fanya anbacho biashara inataka
tumia au fanya ambacho unaweza kukifanya vizuri zaidi usilazimishe kwa kutaka
kuonekana unajua sana au unaweza kufanya kuliko wengine ila fanya kwa kuangalia
ni kipi unaweza kukifanya vizuri zaidi ya vingine na kazi nyingine waachie
wengine wafanye kwa upande wao kila mtu afanye kazi ambayo anaiweza na anaimudu
ipasavyo na biashara itafanikiwe usiwe mchoyo wa kazi au nafasi sababu ya
kufikiria unapunguza faida, faida inakuja katika ufanisi wa kazi na utendaji wa
kazi unaweza kuwa ndio unafanya kazi mbili kwa ufanisi na ufasaha lakini kila
kazi ikikuhitaji kwa wakati mmoja utafanyaje?
Njia yako kubwa ya kuongeza mafanikio iko wapi?
Kuna wafanyabiashara
wanafanya kazi bila hata kujua ni biashara ipi inawapa nafasi katika soko la
ushindani na mafanikio ya biashar a zao, wao wanachojua ni kifanya kazi na
kupata kiasi na kukichanganya basi wanaendelea na maisha lakini iwapo unataka
biashara yako igfanikiwe kwa kiwango unachohitaji basi hakikisha unatambua vitu
kama hizi ni muhimu sana kwako na
biashara yako tambua upenyo wako wa kupitia na njia za kuupitishia huo upenyo
na mbinu zake .
Utajisikiaje iwapo
utakuwa na uwezo wa kuongeza wateja wako kwa asilimia 20% kupitia mtandao wa
kijamii na internet,Vipi kama unaweza kutengeneza bidhaa au huduma mpya ambayo
utakuwa na uwezo wa kuongeza bei kwa 15% zaidi? Ni vipi kama unauwezo wa kuongeza
bei zako kwa 20% bila kupoteza wateja
wako?
Kukua na kuongezeka
kwa uhitaji wako unachangiwa na nini? Maongezi?,Masoko?,Bei? Au kitu kingine?
Zifuatazo ndio hatua
za kutambua na kuyafuata mafaniko
makubwa
- Tafuta ni sehemu gani inayotoa nafasi ya kukua na kuongeza kwa biashara yako ?
- Angalia kama unaweza kutumia hiyo nafasi kwa mafanikio ya biashara yako au unahitaji mkufunzi kuja kukusaidi a kukuonyesha njia na kuwahisha,kurahisisha na kuifanya njia ya mafanikio zaidi
- Fanya kitu kuhusiana na hilo .
Watu wengi huogopa
kwenda kwa wataalam na washauri kwa kuhofia gharama na uhakika wa huduma
watakayoipata japo ni kweli wapo washauri na watoa huduma ghali sana lakini
nakupa siri hakuna alighali halafu hana huduma ya watu wasio na uwezo wa
kumlipa nenda mfate atakusaidia kwa uwezo wako usiogope , usijihisi unajua kila
kitu jifunze kupitia wakufunzi na pia watafuta pale iakapokuwa ni msaada kwa
ajili ya biashara yako.
2.Ili kufanikiwa nahitaji (hakuna) katika biashara yangu
Endelea kujifunza
vitu vipya kila siku , fanya kazi mara nyingi uwezavyo ili ufikie malengo yako , mafanikio ya
biashara hayaji kama hauyatafuti tena
sio kuyatafuta tu ni kuyatafuta kwa bidii, na sio kuyatafuta kwa kutapatapa
unatakiwa kuwa na biashara ambayo utaifanya kwa muda wako na moyo wako wote
ndio hiyo itakayo kufanikisha unatakiwa hiyo biashara kuisukuma na kuisukuma
hadi inatengeneza msingi wake . Hivyo hutakiwi kujiamini na kusema eti
hauhitaji chochote katika biashara yako ili ufanikiwe ukiwa unamaanisha vya
kukufanya ufanikiwe vyote unavyo huo ni uongo na sio kwamba hauna kitu
kilichopungua katika biashara yako ila ni kwamba haujui biashara yako,japo
biashara ni yako lakini haujui misingi yake
na anfasi yake katika soko ila unaangalia ni imeingiza kiasi gani yaani
wewe ni sawa na yule mtu anaetoa 10000/= kufanya kazi ya malipo ya 15 na
kufanya matumizi ya 16,000 na mwisho akasema biashara imemlipa kwa vile tu pesa
aliyotumia ni 10,000/= aliyoitoa . Urudie sana na kuusoma huo mfano hapo juu na
jifunze kutenga kati ya faida na mtaji. Usijiaminishe sana labda kuna vingi
ambavyo huvifahamu ila kwa vile haujifunzi ndio maana huvioni jifunze na
kujifunza sana utafanikiwa , na utaona biashara haikamiliki siku zote kwa
sababu kuna washindani, maendeleo , kufeli au kufanikiwa hivyo vyote ni vitu
ambavyo vinasimamia biashara yako.
3.Kung'angania mpango mmoja
Hapa naomba
nieleweke vizuri ninapomaanisha kukaa na mpango
mmoja si maanishi biashara moja, kuna watu wanaweza kuchanganya pale
ninaposema mpango na biashara hautakiwi kubadili biashara lakini unatakiwa
kubadilisha mipango , kuna wafanyabiashara na wajasiriamali ambao wao muda wote
wa biashara zao wanatumia mpanfgo mmoja tu , ndio tunatakiwa kuwa na
mipango ya muda mrefu katika
biashara lakini haimaanishi hiyo mipango
ndio biashara kwamba haitakiwi kubadilika fanya biashara kwa kuangalia na
mabadiliko ya nyakati sio kufanya tu kwa
vile ni biashara na umeshaambiwa
inatakiwa iwe hivyo basi na wewe unafanya hivyo hivyo tu muda wote ni
lazima uwe na kipimo chake, biashara inahitaji vitu vingi ili ikupe mafanikio
yanayotakiwa moja wapo ni kuitambua na kwenda na wakati unatakiwa kwenda na
wakati katika biashara yako na sio kwenda na mpango ambao unaweza kubadilika
muda wowote .Mipango ni kianzio cha jinsi biashara yako itakavyokuwa ,
using'anganie mpango wako kwa vile tu ni mpango ambao umejiwekea unatakiwa kuwa
ni mpango ambao unaendana na hali ya soko na maendeleo yake.
Asante kaka kwa elimu yako tunazidi kuelimika na kupata mwanga zaidi kuhusu ujasiriamali na biashara, je nawezaje kupata machapisho yako kwa njia ya hardcopy
ReplyDeleteasante sana mkuu nashukuru kwa kupata taarifa kama elimu ninayoitoa inakusaidia na upande wa machapisho katika makaratasi kwa sasa bado sijafikiria japo nimeshapokea maombi niko katika mchakato huo nitakapokuwa tayari nitawajulisha kupitia hapa hapa katika blogu yetu pendwa
ReplyDelete