Jinsi ya kujibrand wewe mwenyewe


Katika matoleo yaliyopita nilielezea maana na faida za branding lakini leo nitaelezea kuhusu brand kwa maana au kwa nafasi ya mtu hivi ni baadhi ya vitu vinavyoijenga na kuitengeneza brand yako.

 

Kusikiliza

  1. Tengeneza maneno ya kuongea kulingana na rika
  2. Toa maoni mara nyingi kwenye mitandao ya jamii
  1. Sikiliza na wengine kwenye  eneo lako la ushindani
  1. Sikiliza viongozi  wa maeneo mengine na angalia ni vipi mawazo yao unaweza kuyatumia
  2. Usisahau podcast

 

Tovuti

  1. Unatakiwa uwe na blogu au tovuti
  1. Iwe na muonekano mzuri
  1. Ukurasa wa "about us" unatakiwa iwe ni wewe pamoja na biashara yako
  2. Isajili tovuti yako na sehemu zinazoshughulika na kutafuta url(top sites)

 

Pasipoti

  1. Fungua akaunti kwenye mitandao ya kijamii

 

Outpost( Muonekano wako kwenye mitandao ya kijamii)

  1. Hakikisha mtandao wako  unaotumia umeandikwa kwenye profile yako (linkeldin)
  2. Hakikisha kila mtandao wa kijamii uliojiunga umeandika jina la tovuti yako
  1. Kutuma barua pepe zikiwa na link za tovuti yako
  1. Usisahau kulike online forums(yahoo,jamiiforum,etc)

Maudhui( Content)

  1. Tengeneza maudhui mapya mara kwa mara
  2. Jinsi wengine wanavyotumia maudhui yako ndivyo wanavyozidi kuiga
  3. Sheria za kijasili
  4. Weka kiasi cha kuandika na "mimi pia"

 

Maongezi

  1. Usifunge chochote ambacho kinaweza kuulizwa
  1. Ukichangia hoja kwenye blogu za wengine inachangia kuamsha  ari
  1. Tumia busara kujibu maswali yenye ufafanuzi wa kina

 

Jamii

  1. Kumbuka jamii na eneo la masoko vinatofautiana
  1. Hakikisha tovuti yako na nguvu zako zinaonekana ni kwa ajili ya jamii
  1. Changia kwenye blogu za jamii na project zao
  2. Shukuru watu mara nyingi kwa muda wao na kukusikiliza

 

Uso kwa uso

  1. Tembea na business cards
  1. Kuwa na uhakika unapokutana na mtu
  2. Nguo na muonekano  pia vinachangia
  3. Uliza maswali kuhusu watu uliokutana nao
  4. Usitafute mahusiano ya kibiashara ,tafuta eneo ambalo mtakuwa mnashare interest (mpira)
  5. Kutanisha macho

Comments

  1. Asante kwa kutuelewesha na nimekuelewa sana katika post za nyuma ila hii ya leo Sijaelewa kitu kimoja hiyo uliyoandika hapo ndio branding? au kuna branding aina ngapi?

    ReplyDelete
  2. Branding ni pana na kubwa sana lakini ninajaribu kuiweka katika nafasi ambayo haitasumbua sana kuielewa na nimeipa aina nne kuna branding ya (Alama,Mtu,Bidhaa na Mfumo) hivyo katika upande wa branding ya mtu hivyo ni vitu ambavyo unatakiwa uvifanye wakati unatengeneza branding yako mwenyewe, mfano: kila mtu hapa duniani anatengeneza brand yake kwa sababu maana nyingine ya brand pia ni Jina halisi lakini sio kila jina ni Brand, Msanii wa kizazi kipya Nasib Abdul wengi hawamfahamu kwa brand ya hili jina lakini nikisema msanii "Diamond" kila mtu atamtambua hata wewe hapo ulipo unatengeneza brand yako mwenyewe,brand ikikua na kuwa kubwa ndio hata watoto wanakuwa wanakufahamu ukipita sehemu unakuwa unajulikana hapo brand yako inakua. sasa kwa upande wa biashara hatufanyi hivyo huku ndio tunatumia njia hizo hapo juu. Asante

    ReplyDelete
  3. Unawezaje kuwa mjasiriamali na kugundua hili ndilo wazo sahihi kwa ujasiriamali wangu?

    ReplyDelete
  4. Somo la kujitambua nimelielezea kuwa ufupi kwenye matoleo yaliyopita, wazo sahihi kwako linatokana na fursa unayoiona na uwezo wa kuathiri soko kama wazo lako haliathiri soko basi bado haujalifanya liwe imara na mimi naamini wazo lako ambalo ni sahihi kuliko yote ni lile ambalo unalipata na unauwezo wa kulifanya wewe mwenyewe mfano: kama wewe ni mwalimu ukipata wazo la kufungua shule yako au masomo ya ziada ni sawa kabisa tofauti na mwalimu kuamua kufungua mgahawa hapo ni vigumu kwa wewe kuimudu hiyo kazi sababu hauna mapenzi nayo.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango