Vitu vinavyotengeneza biashara yenye afya


Kuna vitu vitatu ambayo hutumika sambamba  ili kutengeneza brand yenye afya

  1. Logo - Nembo


Nembo  ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio
Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako , japo nembo (logo) imekuwa ni kitu cha kawaida kwa watu na wengi wanatengenezea mazoea kwa vile kuna fulani katengeneza au kampuni fulani au ukiwa na biashara fulani ni lazima uwe na nembo lakini ukweli na umuhimu uliopo ndani ya nembo ni mkubwa na zaidi inahitajika nembo hiyo itengenezwe maalum kama ambavyo nimeeleza hapo juu utakuta mtu anatengeneza nembo kwa kukopi nembo nyingine hii sio sahihi tengeneza kitu ambacho kitakuwa ni chenyewe na kitakacho kutambulisha wewe mwenyewe katika soko.


  1. Branding- kulijengea jina utambulisho

Branding ni kutengeneza uaminifu na ahadi ya bidhaa yako kwenye akili ya mteja unaemtegemea
Ambapo brand huunganishwa na bidhaa kwa mteja inatakiwa ulijengee jina la biashara yako utambulisho ambao hata mtoto mdogo akiulizwa atakuwa anatambua brand yako yaani iwe na nafasi katika vichwa vya wateja na wateja watarajiwa.

                 3. Identity - utambulisho ( marketing,advertising,publication,sales) 

 

    Hii inamaanisha aina ya utambulisho utakaotumia kujitambulisha, unaweza kujitambulisha kama expert
    Kujitambulisha kama mzoefu kujitambulisha kwa aina ambayo wewe itakupa ahueni na upenyo kwenye soko ulilopo.tengeneza kitu ambacho kitakutambulisha tofauti na wengine au waliotangulia usijiweke kwenye kundi la wote hata kama mnafanya biashara moja kuwa kwenye kundi la yule kwa kutengeneza utambulisho wako mwenyewe

                       4. Kutokubadilika


    Moja kati ya vitu muhimu katika biashara yako ni msimamo na kutokubadilika badilika mabadiliko wengi huchukulia ni kubadili aina ya biashara lakini mabadiliko ni kitu cha kushangaza sana hata kubadilili rangi ya brand yako ni mabadiliko ambayo yanaweza kuleta athari katika biashara yako jitahidi usibadilike, tumia mtu wa grafiti mmoja ambaye unamuamini akutengenezee vitu vinavyokutambulisha katika soko na akuachie vipimo na alama za rangi na mchanganyiko wake ili hata unapoamua kutengeneza aina nyingine ya kitu mfano flier au broshua utakuwa na maelekezo pamoja na vipimo vya mwanzo ambavyo vitakuongoza kutengeneza kitu kingine bila kubadili asili ya kitu hicho, usichanganye changanye na kubadili badili rangi au vitu vinavyokutangaza na vyenye mawasiliano ya moja kwa moja na wateja wako, logo yako inatakiwa ikae hivyo hivyo iwapo utaamua kubadili basi wape muda wateja wako wa kuaizoea alama mpya kabla ya zamani haijapotea . Kutokubaldilika ndio msingi wa uimara wa biashara yako.

    Comments

    Popular posts from this blog

    Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

    Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

    Aina za malengo na mipango