Vitu vinavyorudisha nyuma wajasiriamali/ wafanyabiashara (sehemu ya 2)
Toleo
lililopita nilitoa maelezo kuhusu vitu ambavyo vinarudisha nyuma wajasiriamali
wengi na wafanyabiashara, ambavyo ni vitu vya kawaida na vinafanyika na vingine
hufanyika kimakosa bila hata kujua.
Unapokuwa
mjasiriamali / mfanyabiashara kufeli ni moja ya hatua za ukuaji wa biashara
yako hivyo tegemea kufeli kila unapotaka kukuza biashara yako,na kama kuna
kufeli ambako ni lazima upitie basi lazima kuwe na namna ya kukabiliana na
kufeli huku inatakiwa kila mpango unaoutengeneza uwe na mpango msaidizi wa
iwapo utafeli basi huu utachukua nafasi au iwapo mambo yataenda mrama kwa
upande huu nitafanya hivi au vile sio kufanya tu huku unawaza na kusema MUNGU
atasaidia. Na madhara yote hutegemea
vitu 4 ambavyo ndio vinakuongoza katika biashara yako
- Mipango biashara yako( Business plan)
Baadhi
ya vitu ambavyo huwa vinawafelisha wengi ni pamoja na jinsi ya utengenezaji au ufanyaji wake,
japokuwa mpango biashara ndio nguzo ya biashara wengi hufikiria ni ufujaji wa
pesa na hii ni kwa sababu kitakacho toka ndani ya mpango bishara hakina uhakika na huwezi
kukipa uhakika asilimia 100 tofauti na mawazo yake ambayo ameshajiaminisha
kupitia hayo.
Katika
hili kwa wajasiriamali wengi wadogo na wa kati hutengeneza mipango biashara ya
kienyeji na asilimia kubwa huishia kufeli kwa sababu inakuwa haijakidhi ule
uwezo unaotakiwa, na baadhi ya vitu ambavyo huwafelisha ni pamoja na ufanyaji
wake asilimia kubwa hufeli kwa kushindwa kuelewa mpango biashara
unafanywaje na unatakiwa kuwa vipi hivyo hufanya kwa namna na jinsi vichwa vyao
vinavyowaambia ambapo wengi hukosea, pia hutengeneza bila kutambua aina za
mipango wanayotengeneza utakuta mjasiriamali mdogo ametengeneza mpango
biashara wake na kitu kikubwa alichokiweka ni mpango wa mafanikio ndani ya
miezi miwili ambapo ataonyesha mathalani biashara yake ni ya kutengeneza
vitumbua basi atafanya mara ya kwanza atauza vitumbua kama mama wa jirani yake
ambapo atafanya kupunguza kidogo pesa ya mauzo ili siku ikizidi au kupungua
inaweza kuendana na mpango wake halafu anapiga mahesabu kwa mwezi anajua
atakuwa na kiasi gani na baada ya hapo anaangalia faida atakayoipata basi
kamaliza mpango biashara wake, hapo unajitengenezea mipango feki ya biashara
yako sababu umetengeneza mpango biashara ambao haujakidhi matakwa ya biashara
hiyo, ninapokea maombi mengi ya watu kuwatengenezea mpango biashara lakini
wengi wao huniambia tayari wakiwa na
biashara hapo inamaanisha tayari ulikuwa na mpango biashara lakini
haujakulipa ndio maana unatafuta ambao ni wa kitaalamu, kujitengenezea mpango
biashara mwenyewe bila kuwa na weledi nao ni kuiweka biashara yako
kwenye hatari ya kushindwa, kitu kingine kinachowarudisha nyuma katika hili ni pamoja
na
muda wa mpango kutumika asilimia kubwa ya wajasiriamali hutengeneza
mpango biashara mmoja tu ambao hauna muda maalumu na wengi huuweka kulingana na
soko litakavyoamua kama soko likiukataa basi anaauacha au anabadilisha
biashara tatizo la mwisho kwa upande huu
ni kukosea kutengeneza mpango biashara utakuta mjasiriamali au mfanyabiashara
katengeneza mpango biashara ambao hauendani na biashara yake anabiashara ya
kutengeneza sabuni anafikiria kutengeneza mpango biashara sawa na wa kampuni ya
kutengeneza sabuni ambao wanaifanya hiyo biashara kwa kipindi kirefu hilo ni
kosa kubwa ambalo linaweza kurudisha nyuma na kuifanya biashara yako ishindwe.
Suruhisho: Tafuta watu maalum wenye weledi wa
kutengeneza mpango biashara waeleze kuhusu biashara yako na watakutengenezea kulingana na hali yako, uwezo na soko lako pia ambapo utapata faida ya vingi sio
tu mpango bali hata mchanganuo wa biashara yako kitaalamu, usiogope kuwafuata
kwa kuhisi ni gharama kubwa hata wanaochaji gharama kubwa wana nafasi gharama
ndogo. Kupata maelekezo zaidi kuhusu jinsi ya kutengeneza mpango biashara
fuatilia kwa kubofya HAPA na HAPA
- Muundo wa
biashara yako .
Hapa
pia kunatatizo kubwa ambalo wengi hufikiria na kukumbuka shuka kukiwa kumekucha
wengi wanapenda kufanya biashara au ujasiriamali lakini hawako tayari kufuata
taratibu za kisheria kutengeneza
biashara hiyo asilimia kubwa hawafuati
sheria na taratibu za kufanya biashara hiyo na kwa sababu katika mpango
wa biashara zao hakuna sehemu hiyo hivyo hufikiria kwanza vitu vinavyohusiana
na ofisi zao bila kufikiria serikali pia inautaratibu na mwisho wa siku utaona inakuwa shida kwao
tena kufukuzana na sheria au hata kufunga biashara zao au kupigwa faini kubwa, hili linawarudisha nyuma wengi japo wapo
ambao hawajui hata hatua za kufuata ili kuzihalalisha biashara zao, muundo wa
usimamizi na utendaji kazi pia ukiwa ni mbovu lazima biashara itayumba
hakuna kitu kisichokuwa na heshima au adabu katika utendaji kazi wake hata
unapokula chakula au kutembea kuna vitu ambavyo ni lazima utavifanya kwa sababu
ndio adabu na heshima ya unachokifanya vivyo hivyo na kwenye biashara pia, na kitu cha mwisho ni muundo wa mbinu za biashara
yako kuna watu ambao kazi yao ni kukopi na kupesti ( kurudia kila kitu
kama mtu mwingine) yaani amepata wazo la
biashara kwa kukopi kwa mtu pia mbinu pia atataka kutumia zile zile kwa
kuwa biashara ni ile ile, haitakiwi iwe hivyo ni lazima mbinu zako
zikutofautishe na zikutenge nawengine.
Suruhisho: Fuata taratibu za kisheria kabla ya kuanza
biashara yoyote tambua hatua zake za kuianzisha kisheria wazo lipo tu na wateja
watakuwepo tu aidha ukifata sheria au usipofuata ila usipofuata ni usumbufu na
hasara ambayo unajitunzia. Hivyo fuata taratibu zote za kisheria ili
kuihalalisha biashara yako.
- Kiwango cha
bima yako
Hapa
kuna tatizo kubwa kwa hapa nchini hata bima za magari kwa sasa watu wanakata
kwa kuwa tu ni lazima lakini watu hawapendi na hawajui bima inafaida gani na
inawasaidia nini, Bima ni muhimili wako kipindi cha majanga hebu fikiria
unapopata janga na ndio umewekeza kila kitu chako katika biashara yako ukiwa
huna bima yoyote ni kwamba ndoto na mafanikio yako yote yamefukiwa na janga
lakini hebu fikiria upande wa pili iwapo ukiwa na bima ambayo itakuwezesha
kulipwa na kurudishiwa vitu vyako kama zamani ni kiasi unakuwa unfanya kazi na
biashara yako kwa kujiamini, tunafurahia tu kusikia kuna watu wamekatia bima
hadi miguu yao hiyo ni kwa sababu majanga ni moja kati ya vitu ambavyo
vitakukuta hivyo jiandae kwa hilo kuna usemi unasema usipojiandaa kushinda basi
jiandae kushindwa , Bima ni kitu cha muhimu kwa maisha yako na biashara yako.
Kampuni zipo nyingi tu zinazohusika na hilo bima zipo nyingi na zina faida
kubwa kwako na biashara yako.
Suruhisho: Epuka hasara za majanga kwa kuiwekea bima
biashara yako.
- Kusaini
mikataba
Hili
pia ni moja kati ya sababu zinazowarudisha nyuma wajasiliamali wadogo ,
asilimia kubwa huogopa tarakimu za pesa bila kuangalia gharama husika hivyo
kujikuta wanafanya kazi kubwa kwa malipo kidogo, pia wapo ambao husaini
mikataba kutokana na shinikizo tu aidha hana fedha au biashara haiendi sawa,
wapo ambao wao huangalia faida za muda mfupi na kukurupukia na asilimia kubwa
huwa ni kutokuwa makini na hivyo husaini bila hata kujua wanakubali na kuingia
mkataba wa aina gani.
Suruhisho: Kuongeza umakini katika mikataba unayosaini
usichoke kusoma kwa kuwa tu umepewa baadhi ya faida au madhumuni yake bila
kusoma angalia mkataba unaoingia unafaida gani na unakupa uhuru na madhara gani
kabla ya kusaini.
Comments
Post a Comment