Muendelezo wa hatua za kutengeneza mpango biashara ( Business plan)

Mara ya mwisho tuliangalia hatua sita (6)za mwanzo katika shughuli hii ya kutengeneza mpango biashara (business plan), leo tutamalizia hatua sita nyingine zilizo baki.hatua za mwanzo zilikuwa no pamoja na Jina,Aina ya biashara,Historia ya biashara na maendeleo yake,Huduma/bidhaa,Tathmini ya soko na Ushindani. Leo tutazimalizia zilizobaki kwa kufuata utaratibu.


Masoko


.Katika mpango biashara wako unatakiwa uonyeshe mbinu za
 promosheni na mauzo ya bidhaa/ huduma yako na vitu unavyotakiwa uvitolee maelekezo zaidi ni pamoja na muonekano wa ya huduma/bidhaa yako, utofauti wake, utambuzi wa wateja wako,watu wanaofanya kazi za masoko  na mauzo,mzunguko wa mauzo, aina ya kujitangaza/promosheni, Upangaji wa bei, Ushindani na huduma kwa wateja.


Ufanyaji kazi


Kipengele  hiki unatakiwa uonyeshe uelewa wako wa kufuatilia maendeleo ya huduma/ bidhaa kutoka katika uzalishaji hadi kwenye soko na baadhi ya vitu vya kuainisha ni pamoja na Gharama za mtindo wa uzalishaji, rasilimali, eneo, vifaa, wafanyakazi na upanukaji wa biashara.




Usimamizi wa utawala.


Hili nalo ni jambo nyeti ambalo unapotengeneza mpango biashara wako ni vizuri kuliangalia kwa umakini kwani kipengele hiki kisipokuwa imara vipengele vingi haviwezi kufanikiwa na mambo utakayoainisha ni mtindo wa utawala ( Falsafa), muundo wa kikundi /ofisi mfumo wa ufikishaji taarifa,mitindo ya kuwasiliana, uwezo wa waajiriwa na semina, mahitaji ya kazi,taratibu na mifumo ya usimamizi na sheria na wajibu.



Uwezo wa wafanyakazi.


Hapa ni kuchagua kada gani ya weledi inayohitajika hivyo pia ni lazima uonyeshe weledi wa wafanyakazi unaohitaji na katika kipengele hiki unatakiwa kuonyesha elimu na uzoefu wa mmiliki (wa) na wafanyakazi wake, nafasi /vyeo na kazi zake,Mshahara na marupurupu, kazi na wajibu,malengo na mipango.


Matatizo na utatuzi.


Hakuna biashara isiyokuwa na matatizo hivyo unatakiwa kuonyesha mbinu za kutatua matatizo ambazo hubadili changamoto kuwa fursa. Uwezo wa kubeba matatizo/hatarishi,jinsi ya kutatua ugomvi, washindani wa baadae, matokeo ya kiuchumi na uwezo wa kutatua matatizo ( skill).


Maelezo ya kiuchumi

Kipengele hiki utaainisha uthibitishaji wa fedha,mikopo ya benki, ushuru/kodi, gharama za kuanzia, matarajio ya mapato (miaka 3), mzunguko wa fedha ( miaka 3), mipango ya fedha kwa uthibitisho (miaka 3).



VIAMBATANISHO.

Baada ya kumaliza kuanisha vipengele vyote hapo juu kwa mpangilio huo unamalizia na viambatanisho vya kuupa nguvu mpango biashara wako ambavyo ni picha ya bidhaa/vitendea kazi, nyaraka za kuhalalisha,makubaliano ya kisheria,vifaa vya masoko,utafiti au masomo ya utafiti,utaratibu wa ufanyaji kazi ( mada), chati ya utawala/ofisi, utaratibu wa kazi, Cv na nyongeza ya nyaraka za kifedha.



Iwapo utatengeneza mpango biashara wako kwa kufuata vipengele vyote hapo juu, mpango biashara wako utakuwa ni wa mafanikio na uliopo katika uwezo unaokubalika.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango