BRAND
Brand ni rasilimali
inayotokana na ahadi ambayo inaunganishwa na bidhaa kwa wateja wake.
Shughuli ya brand
inatakiwa iwe imedizainiwa maalum kwa
ajili ya kampuni yako
Kukutofautisha na
wapinzani wako kibiashara. Hata kama wapinzani wote wanamuonekano
Mzuri au kukushinda
wewe .
- Brand yenye mafanikio huzingatia sana umoja
Inapojitambulisha
haijitambulishi kwa vitu vingi
Mfano:1.
Kampuni ya Cocacola wanabidhaa nyingi lakini ukiona matangazo yao
wamejikita sana kwenye
kuitangaza cocacola yenyewe.
- Kuna tofauti kati ya mauzo na kubrand.
Mfano: unaweza kuuza saa ya Rolex dola 100? Ni
kweli inawezekana kuuzwa kwa bei hiyo
na zikauzwa nyingi lakini nini kitatokea
baada ya muda mrefu kwenye brand ya Rolex.
zitatoka rolex za bei ya chini ambazo
zinauwezo wa kuua kabisa soko la rolex za mwanzo
( Hii inamaanisha brand iliyofanikiwa huwa
haionekani kwa kila mtu)
- Kutafuta masoko ni kujenga brand kwenye ubongo wa unaemtegemea.
- Masoko ni malengo makubwa ya kampuni,ndio maana asilimia kubwa ya watu wanaofanya kazi
Kwenye
makampuni lazima huwa wanakuwa
wameunganishwa na sekta ya masoko
- Sasa hivi dunia ya biashara ipo kwenye utaratibu wa kuhama kutoka KUUZA kwenda KUNUNUA.
Na
kuhama huku kumechangiwa na kusababishwa na kubrand.(kujenga alama)
Watu
wa masoko wanamaana zote za jina la kampuni,majina yalivyogawanyika,majina ya
brands na
Majina
ya mamodels ( wanaoigwa) hata brand ndogo ndogo,brand kubwa ,brand rafiki
nakadhalika
Lakini
ukiangalia ndani ya kichwa cha mteja unaemtarajia, hayo yote yanapotea hebu fikiria mteja
Anaongea
na rafiki yake " hivi unaifikiriaje kuhusu hii Basic branding , project mpya ya Legacy impresion
Brand
haina kitu kingine tofauti ila ni neno lililoko ndani ya kichwa na mawazo
lakini ni neno maalum
La
aina yake. Jina la brand ni jina la kawaida kama mengine linalotamkwa kwa
herufi kubwa na kila
Jina
halisi ni brand haijalishi linamilikiwa
na nani mtu binafsi ,kampuni au jamii.
Mfano: Kilimanjaro ni jina la brand inayoongoza
kwa kuuza maji ya kunywa, lakini pia ni brand jina la
Mlima
na mkoa pia.
Kila
jina halisi ni brand, hata wewe pia ni brand na kama unataka kufanikiwa kikweli
kweli kwenye
Maisha
yako unatakiwa kujichukulia wewe mwenyewe kama brand na ufuate sheria ya kujibrand.
Nguvu
za kubrand zinategemea uwezo wa kuchukua na kutumia tabia.
Mfano: mteja anaeingia shoprite kuchukua mkate
na maziwa kawaida huishia kuchukua
bidhaa
kutoka brand mbili tofauti, japo inaweza
kuwa au haipo kuchagua brand ndani ya kichwa
chake .ni
maziwa na mkate vyote ni bidhaa zisizo kuwa na tofauti sana.Lakini mteja
huyo
huyo akinunua katoni ya bia na sigara
nafasi ya mnunuzi kutafuta brand anayoitaka ni
kubwa. Maana yake ni kwamba mkate na maziwa
ziko katika kundi la kununua bidhaa
lakini bia na sigara ziko katika kundi la
kununua brand
LAKINI UNAWEZA
KUBRAND KWENYE KILA JINA HALISI
Comments
Post a Comment