Jinsi ya kujitangaza na wapi pa kujitangaza

Utafutaji wa masoko umebadilija sana kipindi cha hivi karibuni kutoka mauzo mengi kwa ushawishi wa mdomo hadi kwenye kujitangaza kupitia mtandao.

Asilimia kubwa ya wateja sasa hivi wanapatikana kwenye mtandao na asilimia kubwa ya biashara zinajitangaza kwenye mitandao,hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na upatikanaji wa taarifa nyingi muhimu kwa urahisi.

Njia nyingine inayotumika ni kujitangaza kupitia mteja wako,biashara nyingi sasa hivi ziko kwenye utaratibu wa kutoa kamisheni kwa mteja atakae leta mteja mwingine,kwa sababu marketing ya mteja huwa ya uhakika na ya uzoefu hivyo humvuta mtu zaidi kutumia bidhaa au huduma.

Hivyo ukiangalia njia zote mbili hapo juu ni kama zinaua soko la watu wa masoko badala yake linaongeza soko kwa watu wa teknolojia na habari hali imebadilika hii inakuja pia kama changamoto kwa sekta nyingine ya waliomo ndani ya kada ya kutafuta masoko na wanaofikiria kujiunga yafaa kuangalia zaidi mbele na dunia itahitaji nini zaidi kutoka kwako kwa muda gani.

Hivyo kama biashara au huduma jichunguze unautumiaje mtandao na unawatumiaje wateja wako na hii ya wateja inaenda mbali kidogo hadi kwenye mahusiano, unahusiana vipi na wateja wako unawafanya marafiki au wanunuzi wa biashara yako.

Mabadiliko ya namna ya kutafuta masoko yameenda sambamba pia na mabadiliko jinsi ya kujitangaza na kuuza kutoka kuuza bidhaa hadi kununua huduma au suluhisho,zamani biashara zilikuwa zinauza bidhaa

mfano: Jumbo ni kipodozi kwa ajili ya uso hivyo tangazo lao linakuwa : karibu Jumbo,uwe na muonekano bomba.

hapo inakuwa  ni jumbo anaiuza bidhaa yake lakini kwa sasa hali imebadilika badala ya kuuza faida za bidhaa tena unauza kazi za bidhaa.

Mfano:Jumbo hulainisha ngozi yako na kukuacha mkavu.

Mfano hapo juu haujatangaza bidhaa ila umeelezea moja ya kazi  za bidhaa ambapo wateja wengi sasa hivi ndio wananunua kazi ya bidhaa na sio bidhaa.

Kama mfanyabiashara jitahidi sana kwenda na soko lako na soko la dunia pia.jibrand upate muonekano sahihi ili upate nafasi kwenye soko la ushindani.

Kwa mahitaji ya ushauri , vijarida na maelezo zaidi kuhusu branding wasiliana nami kwa simu nambari 0684047323 au elishachuma@gmail.com.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango