Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Hali ya mzunguko na mfumo wa biashara imebadilika sana hapa nchini na hii imechangiwa na kuongezeka kwa makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakiongeza chachu ya kuendelea kufanya zaidi ya pale wazawa wanapofanya, na tofauti kubwa ambayo inafanya kampuni nyingi na biashara nyingi za nje kufanikiwa ni Branding, asilimia kubwa ya hizo kampuni huingia nchini tayari zikiwa zimeshajibrand hivyo inakuwa rahisi kupata nafasi katika soko la ndani.

Kinyume cha hapo asilimia kubwa ya biashara au kampuni zetu wazawa hazijafanya Branding ambayo ndio uti wa mgongo wa biashara, matokeo yake imekuwa hatuwezi kuuza ndani sababu hazina muonekano mzuri na hatuwezi kuuza nje sababu pia hazijafanyiwa branding nzuri.

Baada ya serikali kuiona changamoto hiyo ikaanza kusisitiza wafanyabiashara kufanya branding vizuri( kuboresha  utengenezaji na upakiaji wa bidhaa uwe mzuri na wa kuvutia ili bidhaa zetu zipate nafasi hata katika soko la nje kwa wingi).

Hivyo mabadiliko hayo yameathiri pia na soko la ndani, kwa vile tunaagiza vitu vingi kutoka nje, vile vinavyotengenezwa ndani vikiwa havijabrandiwa vinakosa soko katika eneo lake la ushindani, watu sasa wananunua brand sio bidhaa ukiwaaminisha bidhaa yako ni bora na akaikuta bidhaa yako ni bora basi utakuwa umempata huyo mteja, Je umejibrand vyema kiasi cha kupata nafasi katika eneo lako la ushindani? una nafasi katika soko lako?

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango