Nembo yako inamaanisha nini?

Je wewe ni mfanya biashara au mjasiriamali au mfanyabiashara?umetengenezaje nembo yako? inakidhdi vigezo vya soko lako?

Kwanza Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi.

Kwanini biashara yako inahitaji nembo
1.Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako
2.Huonyesha muonekano unaotakiwa
3.hukuongezea hadhi
4.huonyesha utofauti wako na wengine katika soko
5.Kuwa na muonekano wa kuvutia
6.Hujipanga yenyewe kwa malengo flani ya soko.

Vitu vya kuangalia unapotengeneza logo
1. Iwe ya kipekee
2. Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma
3. Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea
4. Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda
( isipitwe na wakati)
5. Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja ya mawasiliano.

Ushindani umeongezeka sana kwa sasa, sokoni bila ya kuwa na bidhaa iliyofanyiwa brand vizuri utalazimishwa kufuata wengine, hivyo hakikisha unafuata mtu au kampuni inayofahamu vizuri branding na kudizaini ili wakutengenezee nembo itakayokidhi soko na matakwa yake.

Jipatie muongozo wa biashara na kitabu kipya cha Elisha chuma " Muongozo wa biashara" kitabu hiki kitakuelimisha na kukuongoza jinsi ya kusimamia kutangaza na kuuza biashara yako,kujitambua na jinsi ya kupata wazo bora la biashara kutoka eneo ulipo.kwa booking tuma meseji namba 0713603699

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango