Wazo la biashara 01

Asilimia 80% ya dawa tunazotumia mahospitalini zinatokana na miti,na asilimia 60 ya magonjwa tunayougua yanatokana na mtindo wa maisha, hivyo ukiwa kama mjasiriamali ama mfanyabiashara unatakiwa uone fursa hapo katikati ya kuugua na miti.
Matunda yanatumika sana kama dawa, na chakula ni dawa ndio maana ukikikosea kinakuwa sumu mwilini sasa tupitie fursa hii,ikakufungue na kukupa maono mapya.

FURSA: Unaweza  kuuza ujuzi  ama kuwa mshauri wa masuala ya chakula,matunda na miti.

JINSI YA KUIFANYA: Kama mtumiaji wa mtandao anza kwa kutafuta na soma kwa makini    matumizi,faida,utengenezwaji,uhifadhi na mfumo wa mwanadamu unavyopokea na unatumia nini kwa matunda ambayo yanapatikana sana eneo lako ama yanayopatikana kwa urahisi ( Mfano kuchanganya tunda lenye ukali na lisilokuwa na ukali unaliua lile tunda lisilokuwa na ukali linakuwa pombe(Nanasi na ndizi).),fuatilia na chakula uandaaji,viungo,upishi na kadha wa kadha hakikisha unatambua kila aina ya chakula tunda na miti kazi ambazo zinaenda kuifanya mwilini.

Kisha panga vizuri maelezo yako kwa kufuata mtiririko mzuri,anza kwa kufungua akaunti kwenye mitandao ya kijamii na utoe elimu, unaweza kutoa nusu ili mtu akitaka kujua dozi ama ale vipi inabidi akutafute weka malipo kidogo ili iruhusu watu wengi kukutafuta na kukutengenezea jina.Pia unaweza kufungua blogu ambayo utakuwa unatoa mafunzo kulingana na aina ya unachokitaka kukiweka, hapo utauza eneo kwa ajili ya matangazo ya watu wa wanaoendana na kada yako, wauza matunda, wauza chakula na kadha wa kadha, ama unaweza kujisajili na google adsense nao wataweka matangazo yao utakuwa unalipwa kwa watu kuingia katika blogu yako ama kubofya eneo lilipo tangazo lao.

CHANGAMOTO: Upatikanaji wa hayo maelezo na yawe maelezo ya kina na ya ukweli, kutokutegemea kupata matokeo chanya kila utakapo tafuta hayo maelezo,itakuchukua muda hadi kukamilisha,Inahitaji kueleza kwanza kabla ya kukubaliwa.

WASHINDANI: Vituo vya afya ya miti shamba, Dokta,Watu wanaojihusisha na mambo ya asili,Mtu aliesikia wazo hili na kuamua kulifanyia kazi kama wewe.Mtu aliekuwa na wazo lakini alikuwa na uoga wa kulifanya.

BAJETI: Tenga bajeti ya vitu vifuatavyo,Usafiri,Sehemu ya kutunzia (Maelezo),Mtandao,Simu yenye uwezo,Kompyuta.

Muhimu: Usilichukue wazo kama lilivyo na kwenda kulitumia angalia kwanza kama linaendana na wewe na linakufaa ama limeendana na wewe ,tafuta njia ambazo ni rafiki na wewe ili ulikamilishe usikariri nilizoandika.Pia fanya kwa moyo mmoja usitegemee malipo ya haraka hii inahitaji muda na umakini.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango