KANUNI YA KUFANIKIWA NA FEDHA



Haya maneno yamezoeleka kutumika na yamekuwa ya kawaida sana japo yanamsingi mkubwa katika mafanikio yetu ya kila siku,kuna baadhi ya mambo tumeyageuza juu chini ambapo kwa sasa yanatusumbua sana kiimani,kiuchumi na hata kielimu,hebu angalia hiyo formula hapo juu,iko hivyo katika maisha yako?

Nitairudia tena kisha nitaidadafua ili uelewe na kisha uone unakosea ama tunakosea wapi katika kutengeneza pesa na mafanikio kwa ujumla formula inasema

FEDHA = SHUKRANI,SHUKRANI = BARAKA. Kwahiyo BARAKA = FEDHA

Kiuhalisia na mtindo wa maisha tuliochagua aidha kwa kurithi ama kuamua ni kwamba formula iko kinyume FEDHA = BARAKA, BARAKA zinatoa SHUKRANI,ndio maana mafanikio ya watu wengi yanakwama kwa sababu ya kugeuza kanuni ya mafanikio unakuwa unajali zaidi kupata pesa kuliko baraka ambazo ndio chanzo cha fedha zenyewe haya tuipitie kanuni hapa chini utakubaliana na mimi.

FEDHA = SHUKRANI ( Malipo ya kazi ama kitu chochote unachokifanya ni shukrani ya kile ulichokifanya wala sio wajibu wala si lazima yale malipo yafanyike ila ni kwa shukrani za yule ulimtatulia tatizo mfano katika biashara kuna mfanyabiashara na mteja siku zote kazi ya mfanyabiashara ni kutatua matatizo ya mteja wake yaani mteja anatatizo la unga,mfanyabiashara atamletea na atampatia ile fedha unayopokea ni kiwango cha shukrani kwa kutatua tatizo lake sasa ukiishi kwa kuangalia fedha na sio utatuzi mafanikio yako yatakuwa madogo sana,hivyo ile pesa ama malipo yoyote unayopokea ni shukrani ya kutatua tatizo na mara nyingine inaweza kuwa hata sio mteja mtu yoyote wa kawaida ila ukitatua tatizo lake anakupa shukrani ya fedha,sio kama unahaki ya kupewa hiyo shukrani ndio maana shukrani huwa haitoki mwanzo ila mwisho.sasa basi kuna watakaosema mbona huwa kwenye kazi malipo huwa ni kwa makabaliano na yanafanyika vivyo hivyo.Makubaliano ya kazini ni makubaliano ya kusaidiana kufikia lengo la kutatua tatizo na shukrani yako itakuwa kiasi kadhaa,mifano ni mingi lakini mwisho jibu ni kwamba malipo yako ni shukrani ya kutatua tatizo haijalishi ni kwa aina gani kitambo kipindi cha batter trade (biashara ya kubadilishana) ilikuwa bado fedha haijapewa mkazo shukrani ilikuwa ni kitu kwa kitu na huu ndio ulikuwa msingi mkubwa wa Fedha hata ilipoanzishwa kuwakilisha shukrani.

SHUKRANI = BARAKA - haya hatua ya pili ya kanuni inasema Shukrani ni sawa sawa na baraka,kwanini inakuwa hivyo kwanza kabisa unatakiwa utambue kuna aina nyingi za shukrani na zote hizo zinategemeana na aina ya makubaliano ya utatuzi,shukrani (ya fedha unayopewa kwa makubaliano) huwa inakuwa imefungwa tayari kukutengenezea baraka nyingine kwa sababu ni ya makubaliano na unaitegemea lakini shukrani ya kutatua tatizo na ukapokea fedha,maneno ama kitu chochote inatengeneza baraka katika kile unahokifanya na kuendelea kupata ufumbuzi na utatuzi zaidi ili upokee shukrani za makubaliano nyingi zaidi,nadhani unaanza kuipata picha ya huu mzunguko wa shukrani na baraka ,hivyo jitahidi kufanya utatuzi wa changamoto bila makubaiano na baraka zako zitakuwa nyingi.

BARAKA = FEDHA - hii inaanza na kwahiyo nikiwa namaanisha baada ya kuufanya mzunguko wote huo utatambua kama Baraka ni sawa sawa na fedha kwa sababu ili upate Fedha ni lazima utatue tatizo ama ili utatue tatizo ni lazima uwe na baraka ndio upate shukrani.kitu ambacho kiko tofauti san a na jinsi tunavyoishi.Fedha imechukua nafasi kubwa ya baraka zetu.

Umeshawahi kujiuliza unapata amani na faraja kiasi gani kwa kumsaidia mhitaji?,kutatua tatizo la mtu asiekufahamu  na akawa anakushukuru ama mtu anaekufahamu lakini haukuwa na miadi nae ya kumtatulia tatizo,huwa kuna ile furaha ya ndani ambayo huwa haielezeki kwa wote ulimtatulia hukunenea mazuri na wewe ulietatua huwa na amani na furaha moyoni.iko tofauti sana na unapofanya kitu kwa kutegemea kupokea kitu hata unapopokea shukrani huwa haina nguvu pande zote 2 na hii ndio chanzo cha wewe kubaki hapo ulipo.

Katika uchumi mafanikio sio ya mtu mmoja bali ni ya kwake na wanaomzunguka,ukifanikiwa mwenyewe na wanaokuzunguka hawajafanikiwa bado italeta shida kwa wewe kuendelea kufanikiwa na hii inachochewa na ubinafsi na umimi,lakini ukifanikiwa wewe na wewe ukawafanikisha na wenzako baraka zako huwa nyingi ambapo hutengeneza utatuzi mwingi zaidi na mwisho utapokea shukrani zaidi sababu ya baraka za wale watu uliokuwa nao na ukawatatulia matatizo yao.

Hivyo katika maisha kila siku jitahidi kumtatulia tatizo mtu mwenye uhitaji asante yake ni baraka kwako,usifanye katika maisha yako shukrani ya msingi ni pesa peke yake,chukua yoyote lakini tatua tatizo kwa moyo mmoja baraka zake zitakuja kwa wingi hapo mbeleni.ama kwa lugha nyingine fanya utatuzi wa tatizo kwa uaminifu na usifanye kwa ajili ya malipo ya pesa peke yake malipo ya asante yananguvu kuliko malipo ya pesa sababu pesa ukipokea sio ya kwako lakini malipo ya asante ni thawabu na yanadumu kwa muda mrefu. PESA ISITAWALE MAISHA YAKO ILA UTU,UTAFANIKIWA KITU AMBACHO UNAUWEZO WA KUKITOA BURE USIKILIPISHE THAWABU YA ANAEKITUMIA ZITAKULETEA PESA WEWE.ILA UKIHANGAIKA KUTAFUTA PESA AMA UKIJALI ZAIDI MATOKEO YA UFUMBUZI NA SIO BARAKA ZAKE UTAISHIA KUZIPATA CHACHE AMBAPO UTABAKI KUWA MASIKINI SIKU ZOTE.Hii ni moja ya siri ya watu wengi waliofanikiwa na wanaofanikiwa husaidia zaidi kutafuta ufumbuzi ili baraka ziwaongezekee.

mara zote unapokuwa kazini ama unafanya kitu chochote ikumbuke kanuni na iwe ni muongozo wako utafanikiwa Fedha = Shukrani,Shukrani = Baraka, Baraka = Fedha.Hivyo ongeza bidii kuzitafuta baraka ndio kiini cha pesa,wekeza nguvu zako kwenye utatuzi ili upate baraka za kutatua ndipo shukrani ya pesa itakuja kwako.

Tukutane makala ijayo.......................

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango