Aina ya malengo ya kujiwekea unapomaliza mwaka

 Wengi wetu inapofika mwisho wa mwaka hufikiria kuanza upya na kurekebisha sehemu tulizokosea ili mwaka unaofuata uwe wa mafanikio zaidi ya ule unaoishia ama kupita lakini malengo yetu huwa yanajichanganya sababu ya kukosa muongozo thabiti wa kuyafikisha mahala pake na mengi huishia kuwa matarajio ambapo matarajio yasipo kutana na malengo yanakuwa mawazo,wengi tunaangukia kwenye mawazo sababu hatupangi leo nakupa malengo ambayo unapomaliza mwaka hakikisha umeyaandika ili kukukuza wewe,biashara,kazi,imani na kadha wa kadha.

hakikisha umezingatia maeneo makuu 7 tofauti ya kujiwekea malengo na kuhakikisha kila eneo unaweka mikakati thabiti itakayokuwezesha kufikia hayo malengo yako.

Maeneo muhimu ya kujiwekea malengo ni:

1. Malengo ya Kiroho (Spiritual Goals)

2. Malengo ya Familia/Ndoa (Family/Marriage Goals)

3. Malengo ya Fedha (Financial Goals)

4. Malengo ya Maendeleo Binafsi (Personal Development Goals)

5. Malengo ya Kimwili/Kiafya (Physical/Health Goals)

6. Malengo ya Kazi (Career Goals)

7. Malengo ya Kijamii (Social Goals)

Jitahidi unapoandika usiruke na kuna malengo ambayo yanachanua na kuwa na sehemu zaidi ya moja ziguse zote kwa undani.

Mfano : Malengo ya kiroho.

- kukua kiimani
- Kufuasa
- kusaidia/Kujitoa n.k

Usijibanie hata kama ni malengo kumi sehemu kubwa jambo la msingi ni uwe na muongozo wa kukusaidia kufanya mambo yako kufikia malengo kwa uhakika na kuongeza bidii ili kuyafikia hayo malengo.

Pia yapo malengo ya muda mrefu na mfupi hivyo yatenganishe,ukiweza tenga kwa miezi 6 ama 3 kulingana na uwezo na malengo yako.

Kumaliza mwaka sio kubadilisha malengo,kama malengo uliyojipangia mwaka unaoisha yatakuwa hayajatimia ni muda wa kutafakari na kuangalia penye tatizo na kisha kurekebisha na kupanga upya,usibadilishe kwa kuwa mwaka umeisha.Tuumalize mwaka salama na Kuuanza salama

Elisha Chuma

#Tukutane2020.


Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango