Hekima ya baba huonekana kwa mtoto

HEKIMA YA BABA HUONEKANA KWA MTOTO

Ukiwa mzazi mara nyingi hupenda kutumia ukali,fimbo na nyenzo kadha wa kadha katika kuwaelewesha watoto wetu Katika makuzi yao.

Lakini leo nakupa changamoto kama mzazi kile kinachoonekana kwa mwanao ndio kile ulichokihitaji.

Nadhana zinasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo lakini mimi ninaenda ndani zaidi ili kujenga zaidi,Hekima ya baba huonekana kwa mtoto,hivyo usipomfundisha hekima yako usitegemee yeye kujifunza kwa dunia.

Wengi tumekulia malezi ya fimbo na ukali kiukweli zinasaidia lakini hazijengi Sana,fimbo zinatengeneza uoga,hofu,kutokujiamini,amri lakini hata uwezo mdogo wa kufikiri,haya na madhara ambayo huonekana baadae Sana hekima ya baba inakua ni uoga,hofu,kutojiamini na kadhalika ambapo vijana wa Leo ndio tatizo kubwa ufahamu ( mentality) zimeharibika tangu wakiwa wadogo,halafu wakifika ukubwani gafla wanatakiwa wajitegemee ni mtihani mkubwa zaidi kwao sababu hekima ya baba imepungua sana, tunakimbilia sana kuwalaumu watoto bila kutafuta chanzo,samaki mkunje angali mbichi.

Haya twende kuangalia kwanini hekima ya baba na sio ya mama,Katika Hili kwanza mtoto anazaliwa Kama mzazi tambua mtoto anaheshimu na kujifunza Sana kwa kule unachokifanya sio unachosema,ndio maana ni rahisi kumkataza na kusha akarudia muda huo huo lakini akaacha kwa kile ambacho umekiachaa.

Hivyo hekima ya baba iko kwenye makuzi take,watoto hurithi 79% ya baba na 21% tabia za mama,hivyo mtoto huiga zaidi matendo ya baba kuliko ya mama,akili ya mtoto moja kwa moja huwa anazaliwa akiwa na ufahamu wa baba ni sauti ya mwisho,kiongozi ,hata wamama wengi hutumia neno "Baba yako akija nitamwambia" na mtoto anafanya hata Kama hajajua,hii ni kwa sababu  mtoto anaiga zaidi na kubeba vya baba.sasa kabla sijaendelea nikujibu kwanini biblia imeandika mwana mwenye hekima humfurahisha babaye,Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.Malezi na makuzi ya mtoto husimamiwa asilimia kubwa na mama yake,kutungwa mimba,kubeba mimba,kujifungua, kunyonyesha,kumlisha na kadha wa kadha hivyo muda mwingi wa mtoto hupokea malezi na makuzi ya mama lakina note hii point."Mwana mwenye hekima" kwanini  awe ni mzigo wa mama wakati amerithi tabia za baba,iko hivi Katika maisha ya kuishi pamoja mama ana nguvu kuliko baba ndani ya nyumba, ukiwa mwanaume baada ya kuwa na mwanamke  ndani anakua na nguvu juu yako atakuchagulia nguo za kuvaa,chakula Cha kula,muda wa kurudi Hadi marafiki wa kuhusiana nao,mwanaume husikiliza tu ni kwasababu mama huwa mkubwa ndani ya nyumba wa kubadilisha tabia na mienendo ya baba ambayo haitaki na baba akabadilika mifano hai ni mingi watu hubadilika baada ya kuanza kuishi na mwanamke Sasa Kama mama ataziacha tabia mbaya za baba na mtoto akaja kurithi Hilo ni tatizo la mama kuziacha kwa baba ndio maana ni mzigo wake.

Biblia imeandika waheshimu baba na mama yako Waefeso 6:2a lakini mstari wa 4 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu Bali waleeni Katika adabu na maonyo ya Bwana"

Biblia inaanza kumheshimu baba sababu amepewa majukumu ya kuwa kiongozi / kichwa Cha familia hivyo mtoto anapozaliwa moja kwa moja anakuja na heshima zaidi kwa baba na ufahamu wake anaiga sana tabia za baba,hivyo hekima yako Kama baba itaonekana kwenye matendo ya mwanao jinsi ulivyo muonesha tabia zako na vitu vya kuiga kutoka kwako.

Kama hekima yako ni fimbo,usitegemee mwanao kuja kuwa na hekima ya uvumilivu,Kama hekima yako ni ukali usitegemee mwanao kuja kujiamini kufanya maamuzi bila kusitasita" Waleeni Katika adabu na malezi ya Bwana"

Kila unachokifanya Leo mbele ya mtoto wako,ndio atakachorudia kesho,hivyo Kama mzazi jitahidi Sana kujenga ufahamu wa mwanao kwa hekima na tabia za ukali na fimbo,wanajifinza zaidi kwa matendo yetu zaidi ya maneno na adhabu zetu.

Anza Leo kujenga ufahamu sahihi kwa mwano,wewe ndio unatengeneza ama kuharibu kesho yake akiwa mtu mzima,uwezo wa uthubutu,Upeo mkubwa ,heshima na adhabu anavirithi kwa kuviona na kujifunza.

Elisha Chuma.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango