Tofauti ya Ukweli na uhalisia

Ishi kiuhalisia endana na uhalisia wako,huenda ukweli unakuvuta ili usimame mahala ama kuonyesha uwezo lakini uhalisia ndio sehemu pekee unayoweza kuwa na amani na kutengeneza mafanikio yako.

Watu wengi wamefeli kwa kuusimamia ukweli kuliko uhalisia mathalani,ukweli ni kwamba unahitaji kula ili uishi uhalisia ni kwamba unahitaji kufanya kazi ili upate hela ya kukuwezesha kununua chakula ili uishi.

Wasanii,wafanyabiashara na watu wengi wamefelishwa sana na hiki kitu na bado kinawatafuna wengi kuung'ang'ania ukweli ilhali uhalisia unakataa ndio matokeo yake unaishi maisha yasiyokuwa ya kwako mwisho wa kuishi hivyo ni kufeli.

Ishi maisha yako ya uhalisia utapata amani ya moyo na ni rahisi kutengeneza mafanikio na mbinu zake ukiwa kwenye uhalisia kuliko kwenye ukweli wako.

#Maishanihayahaya #wakubadilikaniwewe

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango