Logo/Nembo na Biashara yako
Katika matoleo yangu ya nyuma nilielezea vitu
vinavyotengeneza biashara yenye afya na moja kati ya vitu hivyo ilikuwa ni nembo (Logo) leo
nitaelezea kwa undani kidogo maana yake katika nyanja ya biashara na kwanini biashara inahitaji logo.
Logo/Nembo ni nini?
Nembo
ni alama maalum inayokutambulisha sehemu fulani katika jamii, hiyo ni maana ya
nembo kwa ujumla lakini nembo ( logo) maana yake haitofautiani sana na maana ya hapo juu,logo maana yake ni
alama ya utambulisho wako katika biashara ambayo inatengenezwa kwa umakini na
utaalamu maalum kwa ajili ya biashara yako.
Logo/Nembo inamaana gani kwako
Imekuwa
kawaida kwa watu kutengeneza nembo mtu anapomiliki biashara basi anajua kitu
cha kwanza ni nembo japo hajui inaumuhimu gani katika biashara nilishawahi
kukutana na mmiliki wa biashara moja nikamuuliza kwanini ananembo katika
biashara yake majibu yake ilikuwa ni
" kama biashara lazima na mimi niwe na logo, na unapomiliki biashara nembo
ni lazima ndio maana ninayo" nikamuuliza tena inakusaidia nini katika
biashara yako alinijibu " inasaidia
kwenye business card na invoice ndio naiweka pale inanionyesha professional
katika ninachokifanya" hayo yanaweza kuwa ni mawazo yako pia kuhusu nembo
au logo na ukweli ni kwamba hiyo sio maana ya nembo katika biashara yako.
Historia ya Logo/Nembo
Nembo
au logo imeanza kutumika miaka mingi iliyopita ambapo matumizi yake yamekuwa
yanabadilika kizazi hadi kizazi mwanzoni logo ilikuwa inatumika kama alama tu
ya kuonyesha biashara kama ipo bila kuwa na maana nyingine na umuhimu mwingine
.Baadae mambo yakaanza kubadilika zikaanza kutengeneza nembo/ logo ambazo
zilikuwa zinaonyesha kazi ya biashara na kuitambulisha kwa wateja wake peke
yake logo za kipindi hiki nyingi
zilikuwa za kuonyesha kazi za biashara hivyo nembo hizo zilikuwa zinamabo mengi
na zilikwa na kelele ( kwa maana ya kuonekana na vitu vingi ambavyo vinaonekana
katika logo hiyo) hali imebadilika sasa
hivi nembo sio alama ya kuonyesha kazi za biashara tena sasa nembo imehamia
sehemu nyingine kabisa nembo ni alama inayokutambulisha katika wigo wa biashara
.
Kwa
kuangalia baadhi ya mapitio ya nembo hapo juu tangu ilipoanzishwa hadi leo hebu
jiangalie kama mfanyabiashara nembo yako iko upande gani na uko zama zipi ? Na
je uko sawia sehemu uliyopo? Nembo sio alama tu ya kuwekwa katika biashara au
alama ya kukutambukisha kwa wenzako tu nembo inamaana kubwa zaidi ya hiyo
ambayo watu wengi hawajui ila wanafanya tu, nembo yako leo hii inafanya vitu
vifuatavyo katika biashara yako.
Toleo
lijalo nitaeleza logo inatakiwa iweje na uifanyeje ili iendane na wakati pamoja
na soko linavyohitaji.
Comments
Post a Comment