Mambo yanayorudisha nyuma wajasiriamali/Wafanyabiashara
Kuna mambo mengi
ambayo wajasiriamali wengi huyaangalia kama hayana nafasi sana wanapoanza ujasiriamali lakini baada ya muda
na mambo kugeuka ndipo hukumbuka umuhimu wake, na mengi kati ya hayo huwa
yanakataliwa na misemo ya mitaani ambayo huwa inaathari za moja kwa moja au
vinginevyo kwa mfano maranyingi unapoamua kufanya kitu huwa unafuta mawazo yote
ya kufeli ingawa katika hali halisi kufeli kupo katika hilo hilo unalolifanya
na wengi huwa wanatumia msemo wa " unapofanya jambo fanya kwa moyo wote
usiwaze kufeli sababu utapunguza ari" uwezekano ni ukweli ukiwaza kufeli
unapunguza ari ya kulifanya jambo lakini Je unalolifanya linakufeli au halina?
Na je ukifikiria kufeli unapunguza ari kwa kuliogopa jambo au kwa kuchukua
tahadhari iwapo utafeli? .vivyo hivyo na kwa wajasiriamali wengi pia huwa
hawawazi kufeli katika wanachokifanya ni kushinda tu muda wote lakini
ukiangalia ukweli ni kwamba hata katika maisha yao ya kawaida mipango yao sio
yote inayofanikiwa. Utakuta baada ya mjasiriamali au mfanyabiashara kupewa
elimu ya kitu fulani hufikiria kile kitu peke yake bila ya kuangalia vingine mfano: kwa
mjasiriamali/mfanyabiashara aliefundishwa kutengeneza sabuni ya unga
anapohakikisha anaweza kutengeneza ile sabuni bila ya msaada wa mkufunzi basi
huamua kuanza ile kazi kwa mawazo ya kuifanya iwe ndio biashara yake ya
kumpatia kipato na katika mawazo yake
utakuta ni
Mtaji: hela
aliyokuwa anatunza kidogo kidogo kwa
ajili ya dharura/ mkopo au Mshahara wake
Vifaa: atanunua
vichache vya kutosha hela yake kwanza
Kutengeneza: ujuzi
anao mwenyewe hivyo haina gharama
Wateja: majirani
wake eneo analo ishi na wenye maduka ya karibu na yeye na ndugu zake kwanza
Mpango endelevu:
akishauza akapata faida ataongeza kiwango cha uzalishaji
Kwa mjasiriamali
huyu kama unavyoona hapo juu hakuna sehemu ya kufeli, lakini je ni kweli anachokifanya kitafanikiwa ? Hebu
fikiria kwa mfanyabiashara kama huyu hayo ndio mawazo yake na mpango wake kwa
biashara anayoifikiria kuletea kipato je ameangalia na uwezekano wa kufeli
katika anachokifanya hebu fikiria ni athari gani atazipata iwapo Serikali
itakataza kutumia sabuni ambazo hazijasajiliwa sehemu husika? Itakuaje iwapo
vitendea kazi vitakuwa vichache kulingana na mpangilio wake? Itakuaje iwapo
majirani na ndugu hawatamuunga mkono kwa kununua bidhaa yake, itakuaje siku ya
kumaliza kutengeneza sabuni yake mvua ikanyesha ikanyeshea sabuni zote na ni
sabuni za unga? Itakuaje iwapo gharama za utengenezaji zitapishana na gharama
za mauzo? Jibu la maswali yote hapo juu ni moja KUFELI inatakiwa kuchukua
tahadhari zote kabla ya kuanza kitu chochote ndio maana hata katika mipango
kuna mipango ya muda mrefu na muda mfupi yote hii ni kuchukua tahadhari za
jinsi ya kufikia malengo ya mpango mkuu .
Unapokuwa mjasiriamali / mfanyabiashara kufeli ni moja ya hatua za ukuaji wa biashara yako hivyo tegemea kufeli kila unapotaka kukuza biashara yako,na kama kuna kufeli ambako ni lazima upitie basi lazima kuwe na namna ya kukabiliana na kufeli huku inatakiwa kila mpango unaoutengeneza uwe na mpango msaidizi wa iwapo utafeli basi huu utachukua nafasi au iwapo mambo yataenda mrama kwa upande huu nitafanya hivi au vile sio kufanya tu huku unawaza na kusema MUNGU atasaidia. Na madhara yote hutegemea vitu 3 ambavyo ndio vinakuongoza katika biashara yako
- Mipango biashara yako
- Muundo wa biashara yako
- Kiwango cha Bima yako
- Mikataba unayosaini
Hivi ndivyo
vinavyochangia kufeli kwa biashara yako iwapo utaviweka vizuri na kuvisimamia
kwa uhakika basi biashara yako itasimama na kuendelea siku zote, toleo lijalo
nitavielezea hivyo vitu vinne hapo juu kwa undani unakose wapi na unatakiwa
ufanye nini. Mungu akutangulie tukutane tena toleo lijalo, kwa maswali na
muongozo wa mada hii andika maoni maswali au hoja kupitia eneo la comment hapo
chini au tuma email moja kwa moja elishachuma@gmail.com
Comments
Post a Comment