Muendelezo wa umuhimu wa Logo katika biashara yako

Kukutambulisha katika soko

Logo yako ndio inayokutambulisha katika soko la ushindani ,soko la biashara  na hata kwa wateja hivyo logo yako inatakiwa iwe ambayo ni maalum kweli ili utambulisho wako usije kuwa na muonekano mbaya au usiovutia logo yako ndio ambayo inatathminiwa ndani ya soko mtu anapoiona logo yako ndio anakutambua.



Logo ni muongozi wa biashara yako

 kwa sababu unapokutana na mteja ananunua kitu kutokana na utambulisho na muendelezo wa logo ya bidhaa unayotengeneza siku sio nyingi nilipokea simu kutoka kwa mtu nisiemfahamu akawa anataka nimtengenezee logo kawaida yangu huwa ni kupata maelezo nikamuuliza ameipatia wapi namba yangu na aina ya logo anayotaka alishangaa kidogo kuona nakuwa na maswali kumzidi lakini alielewa na kitu alichokuja kunijibu ni aliona business card yangu kwa mtu akawa amependa logo yangu ikawa imemvutia kiasi kwamba akawa anataka nayeye  nimtengenezee nyingine lakini iwe jamii ya hiyo ya kwangu, hivyo logo yako ni muongozo wa biashara sababu ndio kitu anachokutana nacho mteja kabla ya kukutana na wewe.




Kukutambulisha uepo wako.

Logo inatambulisha uepo wako katika kila kitu nembo inachukua nafasi kubwa ya kukutambulisha kuliko hata binadamu nembo unauwezo wa kuiweka sehemu na ikakutambulisha kwa kila anaeiangalia na siku hizi maana ya logo sio kuelezea shughuli unayoifanya ila nembo sasa hivi inachokifanya ni kukumbusha tu na uepo wa biashara miliki ya nembo hiyo ambapo wewe mwenyewe ndio utakaekumbuka ni huduma gani au bidhaa gani unayoihitaji kutoka kwa mmiliki wake mfano: nilimuuliza kuna mtu alikuwa anafanya kazi kampuni  ya mawasiliano nikamuuliza kwanini huwa wanatumia pesa nyingi kuweka matangazo barabarani  lakini wanaweka jina la kampuni na nembo yao peke yao hakuwa na majibu ya kueleweka na mwisho alinijibu hajui , lakini maana ya kufanya hivyo hiyo ni kutokana kampuni inatoa huduma zaidi ya moja hivyo iwapo wataandika ni tangazo la kitu kimoja au kwa ajili ya kitu kimoja basi watakuwa wamefungia uwezekano na upenyo kwa huduma  nyingine ambazo zinatolewa na kampuni  hiyo hiyo.



Kukuza biashara yako

Logo inatumika kukuza biashara yako sababu ndio alama ambayo inakutambulisha katika sehemu zote unazohitajika kuonekana wewe na biashara yako , biashara yako inasubiri nembo itoe utambulisho ndio yenyewe ifanye kazi, hivyo ukuaji wa biashara yako uko mikononi mwa nembo yako ikishirikiana na vingine lakini cha kwanza katika ukuaji wake ni nembo.biashara yako itakua iwapo logo yako itasambaa na kuonekana sehemu nyingi.



Kuongeza ufanisi wa kazi

Logo inaongeza ufanisi  na muonekano wa kazi yako iwapo utaitumia vizuri logo ukiiweka katika kila sehemu ambayo unatakiwa uonekane itakuongezea ufanisi na muonekano wa biashara yako kupitia yenyewe logo inakuwa kama jaji wa jinsi ya ufanyaji kazi wako kama logo yako haijapangiliwa na hainamuonekano mzuri na vitu kama hizo lazima itakupunguzia muonekano wako hata kama ufanisi ni mzuri logo ndio inayotoa  muongozo wako .

Toleo lijalo nitaeleza logo inatakiwa iweje na uifanyeje ili iendane na wakati pamoja na soko linavyohitaji

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango