Vitu ambavyo vinatakiwa vionekane kwenye nembo yako

  1. Iwe ya kipekee

Watu wengi wamezoea kuwa wanatengeneza logo kwa kuigilizia ya sehemu fulani au kwa kufuatisha mfumo wa kampuni fulani , wengine hufanya kama logo nyingine kisa tu ni kwa vile imempendezea machoni kwake au ameipenda bila kujali ujumbe utakaotoka baada ya hapo, nembo yako mara zote inatakiwa  iwe ya kipekee na isifanane na nembo yoyote dunia nzima. Hasa katika soko ulilopo, unatakiwa kuifuata maana halisi ya nembo kama nembo ni utambulisho wako iweje uwe unafanana na utambulisho wa mwingine na iwapo umeigilizia kutoka kwa mwenzako inamaanisha tayari yeye brand yake ni kubwa kuliko yako hivyo ukitengeneza nembo inayofanana nayakwake ni kama vile unamsaidia kumkumbushia watu na kumtengenezea nafasi katika vichwa vya wateja wake. Mfano: leo hii ukipita sehemu ukaona nembo inayofanana na ile nembo ya brand ya cocacola utamkumbuka nini brand ya cocacola au brand ya yule aliyeitengeneza . Ukweli ni kwamba utaikumbuka cocacola na unaweza hata kuanza kujiuliza kama wamebadilisha nembo utabaki na maswali hata baadae unaweza kuigawa hiyo brand kwa mwingine sasa hivi cocacola wamebadilisha nembo wanatumia nyingine inatofauti kidogo na ile ya mwanzo. Tayari kwa namna moja au nyingine umeshaiua brand yako na umetengeneza tangazo la cocacola bila kujua.

  1. Inatakiwa iwasilishe  uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma

Nembo yako haitakiwi kuwa nembo tu kama nembo,kwa vile nimesema hapo juu inatakiwa iwe ya kipekee sijamaanisha basi utengeneze nembo ambayo haina hata kiwango wala haina maana kwenye biashara yako inatakiwa nembo yako iwe na maana ndani yake ambayo maana hiyo inapatikana ndani ya nembo au jina la brand hii inasaidia kutokumpoteza mtu kutoka katika soko ulilopo mfano unahusika na usafirishaji sio lazima kenye nembo yako kuwe na magari, ndege au meli ilikuonyesha kwamba unahusika na usafirishaji unaweza kutengeneza nembo yako ikawa ni duara la dunia na alama ya mshale juu unaoonyesha kuzunguka dunia tayari utakuwa umetoa zile alama halisi kama gari na vyombo vya moto kwa kuweka alama ya mshale tu. Hivyo hakikisha nembo yako inawasilisha unachokifanya lakini sio lazima iwe kwa picha ya  moja kwa moja.


  1. Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea

Nembo sio alama tu unayoitengeneza kukutambulisha tu katika soko inatakiwa pia iwe na mawasiliano na mteja mtarajiwa iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea, mfano kwa mteja ambae anampango wa kusafiri nje ya nchi anapoona alama ya dunia na mshale katika logo yako na jina la kampuni ni comfort Transportation Company tayari kichwani mwake anahisi hili kampuni ni la usafirishaji sio ndani ya nchi tu hata nje ya nchi , hapo tayari kunakuwa na mawasiliano ya alama na hisia kati ya nembo na mteja wako bila ya wewe mwenyewe kuwepo. Nembo yako hakikisha inatosha kwenye macho yote mawili.

  1. Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati)

Nembo yako haitakiwi kuwa ya muda mfupi au ambayo inapitwa na muda unatakiwa kuwa na nembo ambayo inauwezo wa kujisimamia muda wote na inauwezo wa kukaa kwenye soko muda wote bila kupitwa na wakati mfano nembo ya brand ya maji ya Kilimanjaro ni nembo ambayo inaonyesha mlima, japo ni brand ya maji lakini imetumia brand nyingine (mlima) kujiongezea wateja na nembo yake haiwezi kupitwa na wakati hata kama mlima utapunguza theruji na kupungua urefu bado nembo itaendelea kusimama vile vile na haitapitwa na wakati , unatakiwa na wewe nembo yako pia iwe ya namna hiyo isiwe ile ambayo inapitwa na muda .

 
  1. Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja ya mawasiliano


Katika ulimwengu wa utandawazi nembo yako inatakiwa iwe na uwezo wa kuonekana  kwenye kila nyanja ya mawasiliano isiwe logo ambayo ukiweeka sehemu fulani haiwezi kuaksi sehemu ilipo na mazingira yake logo ambayo ukiiweka sehemu inapoteza muonekano wake wa asili, hiyo sio aina ya logo unayotakiwa kuwa nayo au kuitumia kukutambulisha logo yako inatakiwa iwe na uwezo wa kuonekana vizuri kwenye kila nyanja za mawasiliano.

Comments

  1. Asante kwa kutuelimisha na elimu yako je ntajuaje kama nembo imekidhi hayo mahitaji ilhali sina uzoefu na grafiti

    ReplyDelete
  2. unapochagua sehemu ya kufanyia kazi lazima sasa ifikie hatua ya kuuliza uwezo na kazi zilizopita uwezo wa mtu huonekana katika kazi alizozifanya angalia kama kazi zilizopita zimekidhi haja ya maelezo ya hapo juu kama hazijakidhi mdadisi anauelewa gani na anachokifanya na kinaumuhimu gani kwa biashara yako akijibu kwa nafsi yake huyo sio wa kumpa kazi yako, logo unayotengenezewa wewe inatakiwa iwe kwa mawazo ya biashara yako aiangalie biashara yako sio kuangalia uwezo wake wa kuifanya kazi

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango