Majibu ya Maswali 12 yahusuyo Branding
Kabla ya kuingia moja kwa moja katika somo la branding nimeonelea nitoe kwanza uzi wenye maswali na majibu kuhusu branding ili hata kwa yule ambae haijui na anahayo maswali ya msingi anaweza kuelewa na kupata picha ya kitu ambacho ninataka kuanza kukitolea ufafanuzi. Branding inahitajika kwa kila biashara na kila kitu kwa sababu hata wewe pia ni brand.
chini ni maswali na majibu kuhusu Branding
chini ni maswali na majibu kuhusu Branding
- Brand ni nini?
Ans: Brand
kwa maana moja tunaweza kusema ni muonekano wa biashara yako, branding ni
muonekano wako kuhusu biashara yako na jinsi
gani biashara yako inajitofautisha na washindani wenzako,
- Kazi za Brand.
Brand hutambulisha muonekano
,ubora wa kuaminika kwa watu, huku
bidhaa za generic (kawaida)
hazijulikani na haziaminiki ,hata
hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu
Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema
Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa
Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa
kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji
Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa.
- Kwanini ufanye brand
Unafanya
brand kwa sababu unataka kutambulika na kuongeza mauzo , pia ni kutaka
kujitofautisha na washindani wako
- Faida gani unayoipata
ukibrand
Brand
hukutambulisha,Brand hukutofautisha, brand hutengeneza thamani, Brand
hukutengenezea trademark
- Hasara za kutokubrand
Hautajulikana
kwenye soko,mauzo yako hayataongezeka,hautapata nafasi kwnye ushindani
- Mifano ya Brand
zilizofanikiwa
- Steps entertainment (usambazaji filamu za kitanzania)
- Msama promotion (matamasha- dini)
- Cocacola(Vinywaji)
7. Mifano Brand zilizofeli
- General tyre
- TOL
- Tanganyika peackers
- NICO
8. Brand inasimamiwa na vitu gani?
- Nembo
- Brand
- Utambulisho
- kutokubadilika
9. Mgawanyiko wa Brand
- Brand ya mtu
- Brand ya Kampuni/mfumo
- Brand ya Bidhaa
- Brand ya Alama
10. Nianze kufanya nini?
Tengeneza Alama , halafu jibrand uje utengeneze mfumo then bidhaa
11. Tofauti kati ya kampuni na Brand
Kampuni ni jina la
wamiliki wa Brand
Na Brand ni ahadi unayotaka kuiweka kwa wateja wako, (
ahadi ya mmiliki kwa mteja)
Kutafuta Masoko - ni
kujenga brand kwenye akili ya mteja unaemtegemea
12. Tofauti kati ya elimu ya ujasiriamali na branding
Elimu ya ujasiriamali-
ni elimu inayotolewa kwa ajili ya kukutengenezea njia za kujiajiri na
kujiongezea mapato.
Elimu ya Branding - Ni
elimu ya kujua jinsi ya kuongeza mapato na kujulikana kwenye kipengele
chako cha ushindani
Comments
Post a Comment