Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo na vingine vya kutafutia masoko.
Nimepokea maswali
mengi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vitu kama Nembo, Flaya,Tovuti,Broshua na
vingine vingi
logo/Nembo |
poster |
Flyer/Flaya |
Leo nitatoa sababu
chahche kwanini biashara yako inahitaji hivyo vyote ili ifanikiwe kibiashara.
Ukiviangalia vyote kwa juu juu unaweza kuviona sio vya muhimu sana Mfano:
Kampuni kuwa na logo wakati hakuna mtu anaekuja kuulizia logo wala hakuna mtu
anaekuja kununua logo hivyo ni kitu ambacho unatengeneza kwa gharama na
kinaendelea kuwa chako.
Vivyo hivyo kwa
vingine unatengeneza broshua kwa gharama kubwa lakini unasambaza bure kwa watu
na unaweza kumpa mtu hapo hapo akakitupa ,ukiangalia kwa macho ya fedha zangu
nimeziweka hapa kipewe heshima hauwezi kuona ninachokimaanisha.
Kila biashara
inahitaji kuonekana na pia inahitaji kukua bila kukua na kuonekana haiwezi
kufanikiwa hivyo kutengeneza Nembo yako ni kujipa muonekano katika soko na
kutengeneza vitu kama Flaya,Broshua,Poster hiyo ni kukuza biashara hivyo ili
biashara yako ikue ni lazima ufanye vyote malipo au faida za kufanya hivyo
hazionekani kwa muda huo huo lakini zinaweza kuonekana muda wowote kuanzia
ulipo anza kuzitoa, marejesho yake sio ya papo kwa hapo lakini yana faida ya
muda mrefu Mfano: unapotengeneza logo itatumika kwenye kila sehemu
inayokutambulisha kwa muda wote wa biashara yako na ukitengeneza flaya itasomwa
na wengi kwa muda mfupi au mrefu ambapo tayari utakuwa umewafikia watu wengi
bila wewe mwenyewe kwenda kuonana nao mmoja mmoja, hapa chini zifuatazo ni
sababu kwanini biashara yako inahitaji
vitu hivyo.
1.Kuonekana mkubwa na uliojengeka
Unapotengeneza vitu
hivyo vinapokutambulisha sokoni hukuonyesha wewe ni mkubwa na umejengeka ndio
maana hata umeweza kutengeneza vitu hivyo, biashara isiyokuwa na nembo ikienda
sehemu moja na biashara yenye nembo biashara itakayopata kipaumbele ni yenye nembo
ambayo imeonyesha uthubutu hata kwa kujijenga yenyewe.
2.Kuongeza nafasi ya biashara yako kwenye soko.
Ukitengeneza na vitu
vyako vikaonekana sokoni tayari umeipandisha nafasi yako na hadhi katika soko,
ambapo kwa kuwa na vitu hivyo ni rahisi kwa soko kukutambua na kukupa nafasi.
Mfano umetengeneza flaya za huduma yako na kisha ukzisambaza zikasomwa na watu
wengi hao watu ndio watakao kupa nafasi kwenye soko kwa kukutafuta watakapo kua
na shida na hata kama hatakutafuta atakuwa amekuoneza kwenye listi ya biashara
anazozijua zinafanya shughuli hiyo.
3.Kuvutia wateja wengi
Sababu kubwa ya
kutengeneza vitu hivyo ni wateja na unapotengeneza flaya au broshua ni lazima
utaweka dizaini nzuri na maneno ya kuvutia hivyo ni njia rahisi ya kumvutia
mteja kwa kile anachohitaji kutoka katika biashara yako.
4.Kujitengenezea Chapa( Brand) yako.
Brand ni kitu
kikubwa sana lakini pia unapojitangaza na kujipa muonekano ni sehemu ya
kujibrand na unapotoka nje ya ofisi yako ukiwa na vitu vya kuwapa watu nje ya
walioko ofisini hapo ni unaitoa chapa yako ndani ya ofisi na unaenda kuwapa
watu wengine nje hivyo unaitengenezea brand yako muonekano.
5.Kuonyesha unaijali biashara yako
Mara zote mteja
huhitaji kufanya kazi kwa mtu anaejielewa na anaejijali hivyo kufanya hivyo ni
kumpa uhakika mteja na biashara yako kuonyesha unaijali na unaweza kufanya kitu
kwa ajili ya biashara yako mwenyewe hivyo ni rahisi kwa mteja kupata ile hamasa
ya kuamini unaijali biashara yako hivyo hautaweza kumharibia kazi yake.
6.Kuwapa wateja hali ya uaminifu
Katika soko kumekuwa
na makanjanja wengi hivyo kwa kuingia gharama na kufanya hivyo unampa mteja
hali ya kukuamini na kuona uthubutu sababu kwenye flaya au broshua kunakuwepo
na mawasiliano ya wazi na pia kunakuwa na anwani ya sehemu ofisi inapatikana ambapo
nirahisi kwake kuja kujiaminisha kama kweli hata kabla hajakupa kazi.
7.Kukumbukwa
Unapojitangaza na
kuijenga brand yako ni kuingiza brand yako ndani ya vichwa vya watakaoona na
pia kusoma hivyo brand yako itakuwa inakumbukwa kwa vile tayari iko kwenye
vichwa vya wengi.
Itaendelea wiki
ijayo ……………………………….
Bado mnakaribishwa
kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kutuma namba yako na jina lako
kwenda namba 0767603699 ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni
Mabadiliko lazima.
Pia karibu utangaze
nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia
blogu hii.
Comments
Post a Comment