Salamu za Mwaka mpya

Natoa Shukrani zangu za dhati kwa Muumba wa mbingu na nchi kwa kusimamia na kuniwezesha kufika mwaka 2015 najua yote ni mapenzi yake ni wengi walitamani lakini hawajaifikia siku ya leo pia niwashukuru wote walionitumia salamu za heri ya mwaka, nami kwa mapenzi ya dhati nakutakia heri ya kuufikia mwaka 2015. nakutakia uwe ni mwaka wa mafanikio na kufikia malengo yako.

Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wa mafanikio na changamoto pia kwa kila mtu hivyo nimeelezea kwa undani na kwa ufupi kuhusu biashara na ujasiriamali, mwaka huu nitajikita zaidi kwenye jinsi ya kuifanya biashara yako ifanikiwe au njia za kuikuza biashara yako unapoanza au unapoendelea na biashara yako. Branding ni neno ambalo nimeishakulitaja sana katika matoleo yangu na kwa mwaka huu nataka kila msomaji wangu na wote wanaonifuatilia wafanye brand ya biashara zao. 

Brand ni neno la kiingereza lenye maana isiyokuwa na uwezo wa kushibishwa kama lilivyo kwa lugha ya kiswahili ambapo unaweza kuiita Brand kama chapa lakini ki ukweli Brand ni zaidi ya chapa brand ni mhimili mkuu wa biashara yoyote ambayo inaanza au ambayo tayari imeshaanza, 

Brand imegawanyika katika makundi 4

1. Brand ya Mtu
2.Brand ya Mfumo
3.Brand ya Bidhaa
4. Brand ya Alama

Ambapo katika Brand ya alama pia imegawanyika katika sehemu 2 

1. Brand ya alama ya offline
2. Brand ya alama ya online

kuanzia jumatatu wiki ijayo nitaanza kutoa masomo kuhusu brand hatua baada ya hatua karibu pia kwa wale ambao watahitaji kitabu changu ambacho kinaitwa Nguzo 5 za biashara unaweza kuwasiliana nami kwa mawasiliano yaliyopoa chini au katika ukurasa wa huduma zetu 

Asanteni 
Nawatakieni heri ya mwaka mpya 2015
Elisha Chuma
Mshauri wa Biashara

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango