Sehemu ya pili:Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo na vingine vya kutafutia masoko

Pia ningefurahi kupata mrejesho wako (feedback) juu ya uzi ninazotoa  ili nijue pia kama jamii na mlengwa ninaemtegemea amepata elimu unaohitajika,kwa kuacha komenti yako hapo chini kwenye sehemu ya Comment, Asante.


8. Kueleza jina la kampuni yako


Unapotengeneza nembo au unapotoa flyers na bidhaa nyingine inayokutambulisha kwenye soko  hapo ni kuliweka jina la biashara au kampuni yako katika vichwa va wateja wako watarajiwa,ambapo ili mteja akutafute ni lazima awe anakukumbuka au anajina lako ndio anaweza kukutafuta mfano: Unaposikia bidhaa za Azam tayari unakumbuka na SSB Company ( Bakhresa).

9. Kutunza jina la kampuni yako kwa mteja

Mteja mara zote anahitaji kitu cha kumkumbusha ili aweze kukukumbuka hivyo kwa kutoa vitu kama business card, flyer na vingine vya namna hiyo hapo unakuwa unatunza jina lako kwa mtu unaemtegemea na kwa yule uliempata na siri za kufanikiwa katika biashara ni kumfanya mteja akukumbuke kila anapofikiria huduma yako na huduma za pembeni yako.

10. Kuonyesha utofauti na wengine

Katika kila utakachotoa utakuwa unatengeneza cha tofauti na kutoa utofauti kati yako na wengine katika biashara eidha ni huduma au biadhaa,hivyo kutengeneza na kutoa vitu hivyo ni kujitofautisha na wengine kwenye soko ndio maana vingi vinatumika kuelezea bidhaa au huduma na uwezo wa biashara yako katika utatuaji tatizo la mteja wako.

11. Kujitofautisha na washindani

Kama nilivyoelezea hapo juu, mara nyingi unapotoa kama flyer ni lazima unakuwa umeshajua mshindani wako ametoa kitu gani hivyo unapotoa wewe ni sawa na kuujulisha umma wako kwamba wewe uko tofauti na wengine kwa kutoa huduma au bidhaa fulani hivyo wasikufananishe na wengine mfano: Kwenye mitandao ya simu wote wanatoa huduma za kifedha kwa njia ya simu lakini  kila siku wanatoa flyer , posters kwa ajili ya promosheni mpya ya huduma ile ile hapo wanachofanya ni kujitofautisha na wengine.


12. Kusimama katika eneo lako la ushindani

Unapotengeneza vifaa hivyo ni kuonyesha ujasili na uwezo wa kupambana na kusimama katika eneo lako la ushindani hivyo katika soko na biashara yako nayo itajumuishwa katika wanaofanya ushndani katika eneo lako, na ni kitu cha msingi katika biashara inabidi ujulikane ili upate kufanikiwa biashara iliyojificha haiwezi kuendelea hadi utoke na uonekane katika soko ndio utapata nafasi katika soko.


13. Kuendana na malengo yako

Kila biashara inakuwa na malengo yake ya kufikia sehemu fulani  hivyo kwa kutengeneza nembo na vingine vya kutafutia masoko  unakuwa unasaidia kuyafikia malengo kwa wakati muafaka na kwa muda madhubuti matumizi  ya vitu hivi pia yanakupa muongozo wa uko upande gani katika soko, una athari gani katika soko lako je ukiondoka kutakuwa na pengo lolote au ukibaki utakuwa na ushindani wowote hii ni kutokana na majibu ya kutengeneza visaidizi hivyo.

14. Kuonyesha kujitoa kwako

Kila mteja huwa anataka kuona ahadi ya brand ikitekelezwa katika manunuzi yake aidha bidhaa au huduma hivyo kwa wewe kuingia gharama na kutengeneza visaidizi hivyo tayari unakuwa umeonyesha kujitoa kwako katika hilo ili yeye apate taarifa zako kwa muda muafaka na kwa haraka.
 
Hizo ni baadhi ya sababu kwanini unatakiwa utengeneza nembo na visaidizi vya kutafutia masoko kwa ajili ya biashara yako mara nyingi uwezavyo kitu kingine cha msingi cha kutambua ni kwamba matokeo ya hivi visaidizi hayaji haraka kama moto wa gesi mtu anaweza kukisoma leo lakini akakutafuta baada ya miezi hata mwaka lakini pia kuna mwingine akisoma leo anakutafuta leo hiyo hiyo hivyo usitegemee sana  majibu ya haraka  unachotakiwa kukiamini ni kwamba umefanya kwa sababu nyingi chanya na majibu yake yako njiani.


Uzi unaofata nitaelezea kwa undani nini maana na faida za vitu hivyo Nembo n.k kwa kuelezea kimoja kimoja  na kinatakiwa kiweje kwa ajili yako ambae umesoma leo ili usikurupuke unatakiwa utambue tofauti ili ufanye uchaguzi sahihi kwa biashara yako kulingana na muda,eneo na bajeti.

Bado mnakaribishwa kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kutuma namba yako na jina lako kwenda namba 0767603699 ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mabadiliko lazima.


Pia karibu utangaze nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia blogu hii.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango