Maana ya Branding katika Biashara/ujasiriamali wako
Brand
ni rasilimali inayotokana na ahadi ambayo inaunganishwa na bidhaa kwa wateja
wake.Au brand ni alama inayotambulisha nafasi yako kwenye soko lako la ushindani.
Shughuli
ya brand inatakiwa iwe imedizainiwa na kuandaliwa maalum
kwa ajili ya biashara yako kukutofautisha
na wapinzani wako kibiashara. Hata kama wapinzani wote wanamuonekano
Mzuri
au kukushinda wewe .
1. Brand yenye mafanikio huzingatia sanaumoja,Inapojitambulisha
haijitambulishi kwa vitu vingi
Mfano:1. Kampuni ya Cocacola wanabidhaa nyingi lakini
ukiona matangazo yao wamejikita sana kwenye kuitangaza cocacola yenyewe. ikiwa inamaanisha japo wanabidhaa nyingi bidhaa zote zinajitengenezea au zinatengenezewa brand yake yenyewe.
2.
Kuna tofauti kati ya mauzo na kubrand.
Rolex Orijino |
Rolex feki |
Mfano: unaweza kuuza saa
ya Rolex dola 100? Ni kweli inawezekana kuuzwa kwa bei hiyo
na zikauzwa nyingi lakini nini kitatokea
baada ya muda mrefu kwenye brand ya Rolex.
zitatoka rolex za bei ya chini ambazo zinauwezo wa kuua kabisa soko la rolex za mwanzo
( Hii
inamaanisha brand iliyofanikiwa huwa haionekani kwa kila mtu)
3.
Kutafuta masoko ni kujenga brand kwenye ubongo wa
unaemtegemea.
4.
Masoko ni malengo makubwa ya kampuni,ndio maana
asilimia kubwa ya watu wanaofanya kazi
Kwenye
makampuni lazima huwa wanakuwa
wameunganishwa na sekta ya masoko
5.
Sasa hivi dunia ya biashara ipo kwenye utaratibu
wa kuhama kutoka KUUZA kwenda KUNUNUA.
Na kuhama huku
kumechangiwa na kusababishwa na kubrand.(kujenga alama)
Watu wa masoko
wanamaana zote za jina la kampuni,majina yalivyogawanyika,majina ya brands na
Majina ya mamodels
( wanaoigwa) hata brand ndogo ndogo,brand kubwa ,brand rafiki nakadhalika
Lakini ukiangalia
ndani ya kichwa cha mteja unaemtarajia, hayo yote yanapotea hebu fikiria mteja
Anaongea na rafiki
yake " hivi unaifikiriaje kuhusu hii Basic
branding , project mpya ya Legacy impresion
Brand haina kitu kingine
tofauti ila ni neno lililoko ndani ya kichwa na mawazo lakini ni neno maalum
La aina yake. Jina
la brand ni jina la kawaida kama mengine linalotamkwa kwa herufi kubwa na kila
Jina halisi ni
brand haijalishi linamilikiwa na nani
mtu binafsi ,kampuni au jamii.
Mfano: Kilimanjaro ni
jina la brand inayoongoza kwa kuuza maji ya kunywa, lakini pia ni brand jina la
Mlima na mkoa pia.
Kila jina halisi ni
brand, hata wewe pia ni brand na kama unataka kufanikiwa kikweli kweli kwenye
Maisha yako unatakiwa
kujichukulia wewe mwenyewe kama brand na
ufuate sheria ya kujibrand.
Nguvu za kubrand
zinategemea uwezo wa kuchukua na kutumia tabia.
Mfano: mteja anaeingia
shoprite kuchukua mkate na maziwa kawaida
huishia kuchukua bidha kutoka brand mbili tofauti, japo inaweza
kuwa au haipo kuchagua brand ndani ya kichwa chake.ni
maziwa na mkate vyote ni bidhaa zisizo kuwa na tofauti sana.Lakini mteja
huyo huyo akinunua katoni ya bia na sigara
nafasi ya mnunuzi kutafuta brand anayoitaka ni kubwa. Maana yake ni kwamba mkate na maziwa
ziko katika kundi la kununua bidhaa lakini bia na sigara ziko katika kundi la
kununua brand.
Ungana nami zaidi kupitia ukurasa wangu wa facebook : Elisha
Chuma ("like" ukurasa huu na utapata habari zote na machapisho
mara tuu ninapotoa.) Asante
Comments
Post a Comment