Itambue kanuni kuu ya pesa

Kila kitu katika dunia hii kina kanuni aidha unaijua au hauijui, unaitambua au hauitambui leo nitaiongelea kanuni kubwa kabisa ya kwanza ya pesa. Kwanza kabisa nikubadilishe mawazo kuhusu upatikanaji na dhana ya mzunguko wa pesa.

Kwanza ukubaliane na mimi kwanza kuhusu pesa kwamba, pesa uliyonayo mkononi,mfukoni,benki ama sehemu yoyote ile ambayo unaweza kuitoa kama unavyojiita mmiliki ile pesa sio ya kwako sababu kila pesa unayoishika tayari inasehemu au kazi ya kufanya na kama inasehemu au kazi ya kufanya inamaanisha inabidi ile pesa itoke mkononi mwako, hivyo wewe ni muwakilishi tu umeishika kwa muda huo ili uipeleke kwa mwingine, mfano Ukipewa 10,000 sasa hivi unajihisi kama wewe ni mmiliki wake lakini katika ulimwengu wa fedha wewe umekuwa daraja la mzunguko wake, hivyo kama ni daraja inabidi uipitishe ambapo lazima utaitoa na kumpa mtu mwingine hiyo pesa ambae hata yeye akiisha kuishika inakuwa sio yake tena inabidi akaitoe mfano umeenda kununua unga ukampa 10,000 atakurudishia na chenchi lakini kesho yake na yeye ataenda kuitoa kwingine ili apewe tena mfuko mwingine wa unga, mwisho wa mwezi bosi anakulipa tena sababu unafanya kazi kwenye kampuni ya kuutengeneza huo unga hivyo inakurudia tena na mzunguko unaendelea.

Sasa swali linakuja umiliki halali wa fedha uko wapi?

ukiipitia vizuri dhana hapo juu unaweza kuona kabisa ni sehemu gani au ni kitu gani kinaleta uhalalai wa fedha au pesa inahesabiwa yako ikiwa wapi, haya tuwemo tena leo nimeingia ndani kidogo inabidi uishughulishe akili kukiona nnachokuelezea.

Umiliki halali wa pesa uko katika akili na pesa sio yale makaratasi yenye thamani unayoyashika ila pesa ni thamani ya fedha unayoitarajia kuipata ndani ya kichwa chako, hii inakuwaje mfano ingekuwa umiliki wa makaratasi yenye thamani kiuhalisi ndio kuwa na pesa basi kusingekuwa na matajiri waliofilisika, ukiyachukua yale makaratasi na kuyafungia chumbani bila kuyatoa utaendelea kuwa masikini ila unapoyatoa na kuyaweka katika mzunguko ndipo unakuwa tajiri.ndani ya kichwa chako ndipo kuna pesa kila unachokifanya nje huwa kimeratibiwa ndani na kupewa baraka za kufanyika nje kila unachokifanya hivyo, hata kwa pesa ni vivyo hivyo.

Unapotengeneza pesa yoyote unaitengenezea na umiliki wake unatengeneza mfano: Mshahara wako huwa unatambua ukipokea unaenda wapi hata kabla ya kuupata, pesa unayoenda kuipokea huwa umeshatambua matumizi yake hata kabla ya kuishika, kama hali iko hivyo inamaanisha basi umiliki halali wa pesa uko katika akili na uwezeshaji wa kuipata ile pesa ukiisha kuipata inakuwa sio yako tena, kuna mtu mwingine ambae iko akilini mwake anawaza itoke kwako ije kwake na yeye pia ukishampelekea kuna mtu mwingine ambae anaiwazia itoke kwake iende kwake wakati huo huo na wewe unatengeneza au unaiwazia itoke sehemu nyingine ije kwako hivyo hapo tunakuwa tunatengeneza mzunguko wa pesa ambao unaratibiwa zaidi ndani bila kuonyesha mzunguko au uhusiano ila ikifika nje inaonyesha mzunguko wake.

Sasa kwanini wengine wanakuwa masikini na wengine wanakuwa matajiri, hii ni kutokana na ukubwa wa pesa unayotengeneza na kuihalisisha matajiri wao hutengeneza pesa nyingi kichwani na kuzisimamia kama ilivyopangwa hadi kuhakikisha imekuwa halisi na pia hawana mawazo ya pesa ambayo yanaisha ni kama vile mawazo yako katika mstari na mengine hadi hupandiliana tu lakini yote ikiwa ni katika kutengeneza uhalisia wa umiliki wa pesa ambayo ameipanga, masikini vivyo hivyo kwanza huwa na mawazo ya pesa yanayoisha au yasiyokuwa na hakika sana hivyo mda mwingine hufanya kama vile ngoja nijaribu nadhani italipa nadhani itakuwa sawa hivyo anakuwa hana uhakika na atakachokiweka katika uhalisia anajikuta mawazo yanavitu ambavyo ni vikubwa ila anapokea kidogo sababu ya kukosa uhakika na kuifikiria pesa ndogo na matokeo chanya yake.

Ukitaka kutajirika, tengeneza pesa nyingi zaidi kichwani zenye uhalisia kuliko pesa halisi.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango