Jinsi ya kutengeneza matokeo chanya kupitia business card yako.

Je unaitumiaje fursa ya kujitangaza kupitia Business card yako.japo bzcard ni kikaratasi kidogo kinaweza kukupa matokeo chanya zaidi ya vingine kwanza ni kidogo NA pia ni rahisi kukitunza tofauti na vingine hivyo ukikipa muonekano na maelezo sahihi kina matokeo chanya zaidi.lakini tuangalie hapa chini kwann tunakosea.

kwanza Wengi wetu tumefanya business card kama karatasi ya namba tu,Ndio.Kwa nchi zilizoendelea bzcard imebeba namba tu labda na website.lakini kwa huku kwetu hali iko tofauti watu wengi hawakokaribu sana na matumizi ya mtandao zaidi wanatumia mtandao kupitia mitandao ya kijamii,hii inapunguza fursa ya kuitembelea tovuti yako.

Pili asilimia kubwa ya watengenezaji na watengenezewaji huhisi bzcard ni bzcard tu haijalishi,lakini iko tofauti hata dizaini za bzcard zinatofautiana kulingana na kada tofauti tofauti,ukikosea kuitengeneza usitegemee kama atakaeiona atakufikiria kupitia kada yako.Mfano biashara ya chakula ikatengeneza bzcard kama za benki utaigusa ile bzcard unapofikiria contact za benki sio za chakula,hapo inamaanisha umeshapoteza nafasi ya kupata Mteja bila kujua sababu hupata mawasiliano yako kipindi ambacho hana shida NA wewe.

Mfumo wa biashara tumeurithi toka nje unasheria zake na utendaji kazi wake ukiufuata kwa makini unakupa matokeo makini usitengeneze kitu kwa kufuata mkumbo kama ya fulani nzuri NA ww ukafanya,tengeneza makini kwa ajili ya kada yako.

Je ? unajua bzcard za kada yako zinatakiwa ziweje?

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango