Je unafahamu biashara yako inatakiwa iwe na muoneako gani ili iuze?

Serikali ya awamu ya 5 inapeleka mambo kasi na inathamisha katka mifumo tuliyoizoea na kutupeleka katika mifumo mipya, moja kati ya mabadiliko yanayoongelewa sana na yanayohitajika sana ni kukuza pato la taifa na kupandisha thamani ya pesa yetu hii inamaanisha ni kupunguza uagizaji na kuongeza uzalishaji kutokana na hilo serikali inashauri biashara ziongeze kujitangaza na kuuza nje ya mipaka ya Tanzania ili tuongeze kupokea malipo ya Usd kuliko sisi kulipa Usd. 

Sasa basi moja kati ya kada zinazoangaliwa katika hili ni kada ya biashara ambapo inapokea urasmishaji na uboreshwaji wa mipango ya kimaendeleo kwa kasi sana hivyo biashara nyingi ambazo hazikuwa zimejipanga sawasawa kwenda na kasi yoyote nyingi zitakufa, lakini katika urasimishaji huu biashara haiongelei sana bidhaa ila inaongelea vitambulishi vya bidhaa, Katika mkutano wa wafanyabiashara kutoka India uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana rai yao ilikuwa ni kuboresha upakiaji na vifungashio vya bidhaa zetu hivyo kinacholeta shida sio bidhaa ila ni muonekano wa vitambulishi vya bidhaa,hata hivyo leo siongelei sana soko la nje.

Kwa upande wa soko la ndani hivi sasa makampuni ya kigeni yamekuwa mengi kutokana na fursa nauwezo wa utatuzi matatizo husika kuongezeka, hivyo soko la ushindani linaongezeka nchini kutokanana makampuni kutoka nje pia kutafuta kazi ambazo pia makampuni ya wazawa yanazitafuta,shidainayokuja kutokea ni katika urasmishaji au Branding, asilimia kubwa ya makampuni yetu hayafanyi branding ya biashara zake mengi yanachukua chukua vitu vidogo ambavyo vinahisiwa ni vya muhimuna kuvifanya.lakini kama ilivyo maana ya branding ni kutengeneza ahadi na muonekano wa biasharayako katika macho ya mteja hivyo wengi hufeli sababu ya muonekano wao.

Unapotoa businesscard iliyodizainiwa vizuri na kumkabidhi mteja unatengeneza thamani ya biasharayako bila kujua, unapopeleka nyaraka ya kampuni ikiwa imewekwa kwenye headedpaper/ letterheadinaonyesha weledi na thamani yako kwa biashara yako vivyo hivyo pia kwa Company profile.

Makampuni mengi yemetengeneza company profile zao katika mfumo wa kawaida yaani ule wakuprint karatasi kama memorandum halafu anaibind anatoa hii ni sawa lakini inapunguza na kushusha hadhi ya biashara husika, Branding ni muonekano na kama muonekano wako haukonadhifu inamaanisha huwezi kuwa msafi, kama company profile yako haisadifu muonekano wako inamaanisha kuna shida kati ya biashara au muonekano aidha umechukua muonekano sio wako aubiashara haina hadhi ya muonekano unaotakiwa.

Company profile inatakiwa iwe imedizainiwa vizuri yenye muonekano mzuri na inayokutambulisha vizuri,company profile inajumuisha maelezo mafupi ya kampuni, historia ya kampuni, maono namalengo, kazi za biashara husika,urasmishaji, uhalali wa biashara na pia unaweza kuweka wasifu wa viongozi ili kuipa nguvu msomaji aone anafanya kazi na watu wa kiwango gani lakini kama wasifuwako unaonyesha una Phd na company profile yako iko vile unaonekana ni kama vile phd yako ni ya ubabaishaji iwapo umeshindwa ku value muonekano wa biashara yako utaweza ku value muonekanowa kazi unayotaka kupewa?

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango