Mafanikio ya biashara yako na muonekano wake

Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana muonekano wako ambao hutengeneza uaminifu,heshima na kumvuta mteja, iwapo muonekano ukiwa tofauti na lengo mteja husita kufanya hivyo vilivyopo hapo juu, kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinachukuliwa cha kawaida katika kuipandisha na kuipa muonekano biashara yako ni fani ya Graphics design. fani hii kwa sasa imekuwa ni kama imeingiliwa kila anaetumia kompyuta basi anaweza kuwa graphics designer,hili limepelekea hadi sasa ubora wa muonekano na uhalisia wa kwanza wa biashara unapotea.

Nguzo kuu ya Graphics design ni lazima dizaina awe anajua Branding,Maumbo,Mpangilio,fonts na rangi lakini sasa hivi vingi vinapuuzwa na kulifanya soko kuwa la kawaida,Je katika vitambulishi  vyako vyote viko sawa kulingana na maana ya rangi,maumbo,mpangilio na fonts kufuatana na uasili wa biashara yako? Makampuni makubwa husimamia zaidi suala la muonekano wao wanapokupa kazi wanatoa hadi na vipimo muonekano unaotakiwa na vipimo vya rangi ili usibadilishe muonekano wao lakini je biashara yako inafanya hivyo, au leo nembo inarangi ya bluu na kesho ina rangi blu bahari? usifanye au kutengeneza kitu kwa kutaka ufurahie wewe mwenyewe, unapotengeneza kitu cha kukutangaza ni kwa ajili ya mteja wako sio kwa ajili yako,hivyo tengeneza kwa kuangalia mtu wa mwisho atakipokeaje ( Mteja)?.

Je biashara yako inanembo?Vipeperushi?Broshua?Company Profile? na vingine vingi vya kujitangaza na kama vipo ni kwa kukupendeza wewe au mteja unapotengeneza kitu kwa ajili yako ndio utajaza maelezo mengi katika kila kitu lakini ukifanya kwa ajili ya mteja utamfikiria yeye kwanza anahitaji kuona nini katika unachotengeneza, Je unafanya hivyo?leo nitaongelea kipeperushi wengi wanadhana tofauti sana na kipeperushi hulalamika kutengeneza na kisha watu kukitupa.Je biashara yako inacho kipeperushi na kama kipo kinakidhi hadhi na haja za soko, asilimia kubwa hutengeneza vipeperushi kuendana na kipeperushi cha biashara fulani, hapo unakuwa unageza mawazo ya biashara nyingine, usitegemee utaonekana tofauti kwa kuiga mawazo ya biashara nyingine, huwezi kuleta utofauti kwa kugeza katika soko.

Kipeperushi ni karatasi isiyokunjwa iliyodizainiwa vizuri mahsusi kwa ajili ya kukutangaza,na inatumika kuweka umakini kuhusu tukio,huduma,bidhaa au wazo .

Kipeperushi kama kinavyoitwa hutumika kupeperusha habari au tangazo lako na kipeperushi mara nyingi hubeba ujumbe rahisi na mwepesi kufika kwa walengwa,kipeperushi hutumika sana kwenye halaiki ya watu wengi, Vipeperushi havina gharama kubwa na pia ni njia rahisi ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja.

Aina hii ya kujitangaza kupitia kipeperushi huitwa tupa mbali, kwa sababu mara nyingi mtu anaepewa kipeperushi mara nyingi anakuwa kwenye mwendo ambapo akisoma anapomaliza wengi wao huvitupa kwa kuwa ameshakisoma ambapo sehemu atakapo kitupa yeye pia kuna mwingine atakiokota ili aone ni tangazo la nini na yeye atafanya vivyo hiyo akimaliza kusoma hivyo habari inawafikia wengi kwa mtindo wa kupeperusha.

Watu wengi hufikiria kuwa kwa vile vipeperushi mara nyingi hutupwa basi itakuwa ni hasara kwa wao kutengeneza kitu ambacho kitatupwa badala ya kutunzwa, lakini ukitengeneza vipeperushi unakuwa unaitengenezea biashara yako uwezo mzuri wa kuonekana na nafasi katika ushindani, usifikirie kuacha kufanya promosheni ya biashara yako kwa vile tu unaona unapata faida biashara ni matangazo na ushindani hivyo usisitishe hata mara moja.


Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango