Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 2)

2. Anza kujirasmisha

 Kabla ya kuingia sokoni ni vizuri sana ukiwa umejirasmisha nikiwa namaanisha ukiwa umejiweka rasmi kwa kuingia katika ushindani maana biashara ni ushindani usiposhinda basi utakuwa hauna nafasi katika biashara hiyo ambapo kwako ambae ndio mgeni ama mchanga katika hilo usipojirasmisha mapema inamaanisha unaenda kufeli pale utakapokutana na washindani wako ambao tayari wapo kwa muda mrefu na wamejirasmisha ukiingia kichwa kichwa utajikuta unatumia gharama kubwa kupata nafasi katika soko ambapo ilikuwa ni rahisi kwa kujirasmisha na kutumia upenyo wa soko ambao umeiweka biashara yako.

Nnaposema kujirasmisha nnamaanisha ni kutengeneza vitu ambavyo vitakuweka rasmi katika soko, vitakupa uhalali wa kuwa sokoni na baadhi ni vitu ambavyo mteja atahitaji avione mwanzoni pale anapokutana na biashara yako ambavyo kwa ushauri wangu  ni pamoja na

1. Logo ( Nembo)
2. Businesscard
3. Identification( Vitambulisho)
4.  Letterhead( kichwa cha barua)
5.Envelope ( Bahasha)
6. Receipt ( Risiti)
7. Petty Cash Voucher
8.Proforma Invoice
9. Delivery note
10.Tax invoice

Kila kimoja hapo kinamaana yake na kwanini kieandikwa mwanzoni katika kurasmisha biashara,ambapo sasa shida nyingine inayotokea ni kwamba ili upate vitu sahihi ni lazima upate mtu sahihi wa kukufanyia soko la Graphics design limevamiwa na watu ambao hawana weledi wa kutosha kuhusiana na soko hilo hivyo kama anaekufanyia kazi asipotambua kwa undani Brand na jinsi ya kutengeneza brand ni rahisi sana kuishia katika kutengenezewa vitu sawia lakini kwa ajili ya soko tofauti na lako hivyo katika hilo pia inahitajika mtu unaempa kazi uhakikishe amekuelewa unataka nini na anauelewa wa kutosha kuhusu branding. Kwa upande wa branding ya Graphics design wasiliana na BRAND CREATOR.

leo nitaishia hapa toleo lijalo nitaelezea hatua ya 3 katika hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo,ili kuendelea kupata machapisho yangu bonyeza kitufe cha (follow) upande wa kushoto chini na kila nitakapotoa uzi utapata taarifa ama kwa wale walioko katika mtandao wa facebook unaweza kulike page yangu Elisha Chuma, Pia unaweza kuungana nami kwa kundi la whatsapp kwa kutuma namba yako kwenda 0684047323.

 

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango