IPENDE BIASHARA YAKO

Hakuna kitu kizuri kama kuitangaza biashara yako kitaalamu na kwa mvuto zaidi, biashara zote zinalipa ila inategemeana na unaipenda biashara yako kiasi gani, tujenge mazoea ya kurudisha kwa ajili ya biashara mfano, unapotangaza viatu,mafuta ama nguo hata kama sio vya kwako ila ukitengeneza na nembo yako ukawa kila unachopost kinakuwa nayo hautengenezi muonekano tu bali unatengeneza na hadhi pia, asilimia kubwa ya biashara tuzifanye kwa ajili ya vizazi vijavyo pia bila kuwa na msingi hata wa muonekano biashara inamaanisha ukichoka na yenyewe inachoka lakini kukiwa na msingi hata wa page rasmi ya bidhaa ni rahisi kuendelezwa,pia inapoteza uzito unapotangaza unauza kitu mathalani cha laki 1,2 hadi milioni ila umekipiga picha tu na simu yako hata hakionekani vizuri,tengeneza muonekano wa biashara yako leo ili ujisaidie mwenyewe na vizazi vijavyo.

Tengeneza nembo yako vizuri iwe na muonekano thabiti ili ikidhi vigezo za kada yako,dizaini mtindo ambao utautumia kujitangaza ama kukutambulisha unaweza kutumia wa aina moja ama kujitofautisha kila mara, tengeneza utaratibu wa kujitangaza kuanzia muda hadi jinsi halafu anza kufanya matangazo usiyawahishe mafanikio usitafute kupata wateja ndani ya siku ama wiki tegemea branding inachukua muda kuanza kupata wateja inamanisha tayari umeanza kuaminika hivyo inaweza kuchukua muda lakini usichoke fanya na kufanya mwisho wa siku itakuwa sawa.

Nawashauri wote ambao bado wanafanya biashara zao kizamani ni muda wa kuamka sasa anza kwa kimoja baada ya kingine utafika tu,jibrand kwa kiwango ulichopo.

Nimetoa kitabu chenye muongozo wa kwanza kuhusu Biashara,Ujasiriamali na Branding, jipatie kitabu chako mapema ili ufunguke zaidi,kitabu kinapatikana online katika mfumo wa PDF ili kukipata wasiliana na namba 0684047323. Asante

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango