Biashara hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 3)

3. Chagua sehemu sahihi ya kujibrand

Kila biashara inasehemu yake ambayo inajitosheleza hata biashara yako pia inasehemu ambayo ukiiweka inatosha kabisa hivyo chagua kwa makini sehemu ambayo unaiweka biashara yako ili usije kupishana na biashara yako.

Ili kujua sehemu sahihi ya kuiweka biashara yako no lazima utambue vitu vifuatavyo ili kukupa mwanga wa unakoelekea.

1. Aina ya wateja wako
2. Hali zao kiuchumi
3. Wanapatikana wapi
4. Unawapataje
5. Nnatumia mbinu gani?

Ukishayajibu maswali hayo kwa ufasaha utatambua eneo lako ambalo ni sahihi kujitangaza japo kwa hali ya sasa teknolojia ndio sehemu ambayo wateja wengi wanapatikana hata huko pia kuna matabaka, wateja walioko Facebook ni tofauti na wateja walioko Linkeldin na tofauti na wateja walioko Instagram hivyo usikurupuke kwa kufuata biashara ya mwenzako kwamba kwa vile alifanya kupitia kile akafanikiwa na mimi basi nitafanikiwa hapana utafeli sababu kila biashara ina njia zake za kutokea.

leo nitaishia hapa toleo lijalo nitaelezea hatua ya 4 katika hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo,ili kuendelea kupata machapisho yangu bonyeza kitufe cha (follow) upande wa kushoto chini na kila nitakapotoa uzi utapata taarifa ama kwa wale walioko katika mtandao wa facebook unaweza kulike page yangu Elisha Chuma, Pia unaweza kuungana nami kwa kundi la whatsapp kwa kutuma namba yako kwenda 0684047323.



Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango