hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo ( Sehemu ya 1)

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza swali la napotaka kuanza kufanya Branding natakiwa nifanye kitu gani?, kitu cha kwanza ambacho ni msaada mkubwa kwako kwanza unatakiwa uijue Branding yenyewe ni nini, ndipo unaweza kutambua unatakiwa kuanzia wapi kisha ukaelekea wapi, lakini kwa kupunguza muda na kusaidia kuokoa wakati unaweza kufanya hivi.

1. Tengeneza brand plan

Kitu cha kwanza ambacho unaweza kufanya unatakiwa uwe na mpango wa kila kitu unachokifanya usifanye kwa kukurupuka kwa vile watu wengine huwa wanafanya hapana utakuwa unakosea unatakiwa utengeneze mpango wa jinsi ya kujibrand,ili ukuongoze kwa hatua kulingana na soko lako pia malengo na maono ya biashara yako. ukiwa na brand plan itakusaidia kupata mwanga wa nini cha kufanya,wapi na kwanini.

Brand plan inakusaidia wewe mwenyewe kuona mwanga wa biashara yako inaenda wapi inaongozwa na nini na ina sehemu gani katika soko, hivyo unapoitengeneza tayari unapata mwanga wa kutosha wa biashara yako pia inakusaidia kutengeneza bajeti ambayo itaendana na kiwango chako cha biashara na ushindani ambapo itakusaidia kufanya fanya vitu kwa kuangalia fulani kafanya, maana ya kutengeneza brand sio kutumia pesa bila mpangilio ila ni kutumia pesa kwa mpangilio na malengo ya hali ya juu bila kuwa na mpango huwezi kuyafikia malengo halisi.

Brand plan inatengenezwa na mtu maalum ambae anaijua branding kwa uelewa mzuri na mwenye uwezo wa kutambua soko linahitaji nini na kuna kitu gani ambacho kikokwenye wakati sahihi ili brand plan yako ikawe yenye manufaa sokoni, hivyo usifanye tu na mtu yoyote wala usijitengenezee mwenyewe kufanya hivyo ni sawa na ujitekenye mwenyewe halafu ucheke  mwenyewe ukitegemea na wanaokuangalia wacheke.tafuta mtu ama sehemu sahihi kwa ajili ya kutengeneza brand plan yako.

kwa leo nitaishia hapa toleo lijalo nitaelezea hatua ya pili katika hatua 6 za kukuongoza kutengeneza brand yako kwa kiwango ulichopo,ili kuendelea kupata machapisho yangu bonyeza kitufe cha (follow) upande wa kushoto chini na kila nitakapotoa uzi utapata taarifa ama kwa wale walioko katika mtandao wa facebook unaweza kulike page yangu Elisha Chuma, Pia unaweza kuungana nami kwa kundi la whatsapp kwa kutuma namba yako kwenda 0684047323.


Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango