Maana ya Branding kwa mfanyabiashara na Mjasiriamali
Maana ya branding kwa mfanyabiashara
Branding
ni muonekano wa biashara yako kwa mteja unaemtarajia kwa maana hiyo brand
Inahusika
na inanafasi kubwa katika ukuzaji wa biashara yako na maendeleo yake kila jina ni
Brand
lakini sio kila brand ni jina hivyo ili jina liwe brand linahitaji vitu fulani fulani ili kuwa hivyo
Mfano:
Naseeb Abdul ni jina lakini Diamond ni brand.
Ikiwa inamaana ya kwamba ili uwe
na kitu au Uonekane
katika kipengele au sehemu yako ya ushindani ni lazima uwe na brand na sio
jina.Ukiwa
kama mfanyabiashara ambaye unafanya biashara sio kwa majaribio brand ni lazima katika biashara yako
, Brand inatakiwa kuanza kutengenezwa tangia mwanzo wa biashara ili kuipa nguvu ya kuwepo sokoni kwa
muda mrefu na pia kutengeneza kitu ndani ya vichwa vya wateja wako na wateja
unao wategemea
Mfano:
Serikali ilipoamua kuhama kutoka analojia kwenda dijitali kampuni nyingi zilikuwa
hazijajipanga kuwa mawakala
wa utoaji chaneli hizo kampuni zilizokuwepo ambazo zilikuwa
zinasikia ni
startimes na multchoice(dstv) lakini
ghafla yakaanza kutokea matangazo ya
king;amuzi kipya cha digitek, matangazo
hayo yalikaa kwa muda bila ya
kukiona king'amuzi
hicho wala ofisi zao ila tu kwenye televisheni,watu walipata
hamu ya kuwa nacho hata kabla
Ofisi
zake hazijulikani na kilivyokuja kutoka watu walivinunua vingi kwa bei ya juu
hii ni
kutokana tu na matangazo ambayo
yalitoka hata kabla ya king'amuzi chenyewe kutoka.
Maana ya mfano huu ni kwamba
kampuni ilianza Kutengeneza
brand ya bidhaa yao hata kabla bidhaa haijatoka kwa nia ya kipindi cha kuitoa
bidhaa kitakapofika Bidhaa
ipate nafasi katika soko. Hivyo kutengeneza brand tangia mwanzo wa biashara
kuna faida kubwa
Ikiwa
inamaanisha ili biashara yako ikubalike
au ipate nafasi nzuri ya kuonekana
Kwa
mteja wako ni lazima uwe umeibrand, brand iko kwenye kila kitu hivyo unaweza
Kufanya
brand bila kujua kama unafanya brand .
Hivyo
ukiwa kama mfanyabiashara,mjasiriamali au mtu yeyote unaetegemea kuleta au
kuingiza kitu chochote
Chenye
ushindani tengeneza brand ya bidhaa yako unayoileta .
Unaweza
kupata maelezo zaidi kuhusu branding kwenye matoleo yangu ya nyuma pia
nitaendelea kuwafafanulia
Brand
hatua kwa hatua kadri siku zinavyoenda usikose kupitia kwani yanamanufaa sana
kwako na kwa kizazi chako utakachokuja kukifundisha.
Comments
Post a Comment