vitu vya kutambua baada ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali

biashara au ujasiriamali ni ndoto za watu wengi lakini asilimia kubwa husahau vikwazo na vizingiti ambavyo hutokea kabla na baada ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara  toleo lililopita nilielezea vitu unavyotakiwa kufanya kabla ya kuwa mjasiriamali, leo nitaelezea vitu unavyotakiwa kuvifanya baada ya kuwa mjasiriamali .

kuna vitu na mambo mengi ambayo unatakiwa kuyafata ili ufanikiwe katika kila hatua ya biashara au ujasiriamali wako baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na


                                    Baada ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara

                          1. Biashara ni ushindani, na nafasi ya makosa
 
Moja kati ya vitu ambavyo unatakiwa kutambua ni biashara ni ushindani ili biashara
Iendelee lazima ipate ushindani wa kutosha ndipo biashara itakuwa biashara  ila kama
Hakuna ushindani hautakuwa unafanya biashara bali unatoa huduma,mfano kwa kampuni kama
Tanesco wao hawafanyi biashara wanatoa huduma kwa sababu hawana mshindani wa moja moja , katika Biashara kuna aina tatu za washindani kuna washindani wa moja kwa moja ( hawa ni wale ambao wanafanya biashara ka ma ya kwako), wasio wa moja kwa moja ( hawa ni wale ambao wanafanya biashara mbadala wa biashara yako) na wa tatu ni dhahania ( hawa ni wale ambao hawajaanza kutoa huduma au kufanya biashara lakini wana wazo la kufanya biashara kama yako),  kwa  Tanesko wao hawana mshindani wa moja kwa moja ila wana washindani wasio wa moja kwa moja kama wauza jenereta na umeme wa jua. Hivyo katika biashara ushindani ni kitu muhimu ili uendelee unapokuwa mfanyabiashara au mjasiriamali   lazima utegemee ushindani na kila siku angalia vitu viwili kwa makini katika biashara yako wateja wako  pamoja na washindani wako .

Kitu kingine cha kuongezea hapo ni pia ukiwa mfanyabiashara unatakiwa utambue biashara ni nafasi ya makosa, mshindani wako muda wote anaangalia unamapungufu gani ili  atumie mapungufu yako kujiongezea wateja hivyo unatakiwa kuwa makini kuangalia mapungufu ya washindani wako  na pia kuangalia maamuzi yako,mbinu unazotumia kuongeza wateja na aina ya ujumbe unaoufikisha kwa jamii.asilimia kubwa ya washindani hutumia vitu hivyo kuona mapungufu yako.



                                    2. Muonekano wako unaathiri biashara yako 


Ukiwa kama mfanyabiashara au mjasiriamali muonekano wako unanafasi kubwa  sana katika biashara yako na muonekano huu unajumulisha  ,mavazi, matendo na uwezo wako wa kufikiri  mara nyingi akija mtu ambae anahitaji kukudadisi na kujua unafanye biashara yako ni lazima atakuuliza kuhusu matatizo mnayoyapata na njia mnazotumia kuyatatua hii yote ni kuangalia ni kiasi gani unauwezo wa kukabiliana na matatizo na je ni mtu wa aina gani anaeongea nae , hivyo mara zote angalia sana muonekano wako kuanzia kwenye familia yako hadi kwenye jamii  yako ni jambo la kawaida kusikia " ooh fulani ameanzisha biashara fulani " halafu jibu linatoka " mlevi huyo haiwezi kudumu " hii inamaanisha alieanzisha hiyo biashara muonekano wake na jamii inamchukulia kama mlevi  na tayari muonekano huo unaunganishwa moja moja kwenye biashara yake japo biashara sio yeye ila muonekano umemtengenezea. Hakikisha muonekano wako unashabihiana na biashara yako na nafasi uliyonayo katika jamii.

                                            3.Maneno yako ndio biashara yako
 
Kitu kingine kinachosimamia biashara ni kauli, au maneno yako mwenyewe, ukiwa kama mfanyabiashara unatakiwa mdomo wako uwe na nidhamu na uwezo wa kutamka yaliyo ya staha na pia unatakiwa uzijue lugha za biashara ili kutofautisha majibu unayoyatoa nyumbani sio sawa na unapokutana na mteja ,mfanyabiashara au mjasiriamali mwenzako .
  
                                                  4.Sheria za pesa 
 
Ukiwa kama mfanyabiashara au mjasiriamali unatakiwa uzijue na sheria za pesa pia , sheria kuu ya pesa ni matumizi hivyo pesa sio ya kutunzwa ili ikuzalishie nyingine pesa ni ya kutumiwa ili ikuzalishie nyingine, watu wengi huwa wanaamini mtu mwenye pesa nyingi ni yule ambaye akaunti yake inasoma fedha nyingi kwa nji za wenzetu na watu waliondelea sawa lakini kwa wafanyabiashara wadogo na wafanyakazi ni uongo, mfano : utakuta mtu ametunza mshahara wake kachanganya na fedha zake za pembeni akihisi ni hela ya kuweza kuongea na mtu na ukamwambia basi utasikia sasa hivi nnahela  kama millioni 10,20,50,90. Lakini ile fedha ukiingalia kwa umakini sio ya kwake mimi ninaamini kwamba lile karatasi au sarafu unayoishika huwa ni karatasi na sarafu za kuwakilisha thamani tu na ukiwa nalo sio la kwako mfano: umelipwa mshahara millioni 10 ukitoka tu kuwepa tayari inakuwa imeisha hata kabla haujaitoa mikononi mwako  sababu hiyo pesa tayari inamahitaji yake. Kuna  siri moja iko hivi wewe unapofanya kazi ili ulipwe unakuwa unaifanyia mipango hela ambayo atakupa bosi wako lakini pia kuna mtu mwingine ambae pia anakusubiri ukishaichukua hiyo pesa umpelekee  wewe ni bosi wake na yeye pia kuna mwingine ambae akishaichukua hiyo fedha ni lazima amplekee ili aishi huo ndio mzunguko na sheria ya pesa.maana au nia ya kukuambia hivyo ni ukiwa mfanyabiashara au mjasiria mali ifanye hela yako izunguke  isiwe ya kukaa  na kuhesabiwa tu.

                                                         5. Usiwe na tamaa

 Ukiwa mfanyabiashara au mjasiriamali unatakiwa  usiwe mtu wa tamaa, mtu ambae ukitamanishwa kitu mara moja umeshakitamani na unataka kuwa nacho hiyo ni mbaya kwa sababu ukiwa kwenye biashara utakutana na  wafanyabiashara wengi na wa aina tofauti kuna wengine watakushawishi ujiunge na biashara zao, kuna wengine watakupa mawazo ya biashara nyingine inaweza kuwa ni kwa nia nzuri au mbaya lakini kitu kikubwa na cha msingi ni usiwe na tamaa simamia biashara yako hadi uhakikishe imefikia hatua uliyokuwa unaiota hapo ndio unaweza kuanza kufata ndoto za watu wengine .

                                                6.Fanya biashara yako kwa mipango
 
Usifanye biashara kwa kupelekwa pelekwa panga mipango yako kabla ya kuanza kitu chochote na katika hiyo mipango usisahau kuweka plan b, ukiwa unapanga biashara yako kwa mipango itakupunguzia kuyumba kuyumba na pia kuyaona mafanikio au kushindwa kwa biashara mapema.

                                          7. Brand biashara yako kwa hatua uliyopo.
 
Brand ina maana nyingi na ni kubwa lakini kwa ufupi ni Brand ni muonekano wa bidhaa yako na ahadi uliyoweka kwa mteja unayemtarajia ,lakini brand pia imegawanyika katika aina kuu nne ambazo ni alama , mfumo,mtu  na bidhaa ambavyo vyote hivyo hufanya kazi pamoja ili upate  mafanikio na majibu unayoyataka katika biashara ( nitaelezea siku nyingine kuhusu branding) hivyo kwa kuwa brand ndio msingi wa biashara na kuifanya brand kubwa ni gharama unatakiwa uifanyie brand yako kwa kila hatua unayokuwepo mfano: unaweza kuwa na kampuni ya kuuza kutengeneza unga lakini kwa kuanza hauna fedha ya kuibrand biashara unaweza kuanza kwa kufanya brand ya alama kwa maana ya muonekano wako kwa wateja wako, ukatengeneza nembo pamoja na vitu vichache vya kutumika ofisini baada ya hapo ukachapisha na mifuko ya kuwekea unga tayari hapo unafanya brand ya bidhaa yako ukimaliza hapo utakuwa unauza hadi ukiona unahama sehemu ya kwanza unaweza sasa kutengeneza mfumo kwa wafanyakazi wako kuwavalisha sare na baade pia kuanza sasa na kujitangaza hata kwenye mabango ya barabaani na kwenye runinga.


Comments

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli Mr. Silas ili uwe mjasiriamali unatakiwa kuwa jasili sana sababu kuna mambo mengi ya kutataua na vizingiti vya kupita lakini kuwa jasiri peke yake hakutoshi kukufanya uwe mjasiriamali kuna vitu ambavyo ni muhimu kuvitambua kabla haujaanza ujasiriamali ili vikuongoze katika ujasiri wako na kukamilisha ndoto yako

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango